Acts 24:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya siku tano, kuhani mkuu Anania aliwasili Kaisarea pamoja na wazee kadhaa na wakili mmoja wa sheria aitwaye Tertulo. Walimwendea yule mkuu wa mkoa wakamweleza mashtaka yao juu ya Paulo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya siku tano, kuhani mkuu Anania akateremka hadi Kaisaria pamoja na baadhi ya wazee na mwanasheria aitwaye Tertulo, wakaleta mashtaka yao dhidi ya Paulo mbele ya mtawala.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baada ya siku tano, Anania, Kuhani Mkuu, akatelemka na baadhi ya wazee pamoja naye, na msemi mmoja, Tertulo, nao wakamweleza liwali habari za Paulo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku tano baadaye Anania, kuhani mkuu, alikwenda mjini Kaisaria. Aliwachukua pamoja naye baadhi ya viongozi wa wazee wa Kiyahudi na mwanasheria aitwaye Tertulo. Walikwenda Kaisaria kutoa ushahidi dhidi ya Paulo mbele ya gavana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya siku tano, Kuhani Mkuu Anania aliwasili Kaisarea pamoja na wazee kadhaa na wakili mmoja wa sheria aitwaye Tertulo. Walimwendea yule mkuu wa mkoa wakamweleza mashtaka yao juu ya Paulo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya siku tano, kuhani mkuu Anania aliwasili Kaisarea pamoja na wazee kadhaa na wakili mmoja wa sheria aitwaye Tertulo. Walimwendea yule mkuu wa mkoa wakamweleza mashtaka yao juu ya Paulo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya siku tano, Kuhani Mkuu Anania akashuka akiwa amefuatana na baadhi ya wazee pamoja na mwanasheria mmoja aitwaye Tertulo, nao wakaleta mashtaka yao dhidi ya Paulo mbele ya mtawala.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya siku tano, kuhani mkuu Anania akashuka akiwa amefuatana na baadhi ya wazee pamoja na mwanasheria mmoja aitwaye Tertulo, nao wakaleta mashtaka yao dhidi ya Paulo mbele ya mtawala.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baada ya siku tano, Anania, Kuhani Mkuu, akateremka na baadhi ya wazee pamoja naye, na msemi mmoja, Tertulo, nao wakamweleza mtawala habari za Paulo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya siku tano, kuhani mkuu Anania aliwasili Kaisarea pamoja na wazee kadhaa na wakili mmoja wa sheria aitwaye Tertulo. Walimwendea yule mkuu wa mkoa wakamweleza mashtaka yao juu ya Paulo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku tano zilipopita, mtambikaji mkuu Anania akatelemka pamoja nao wazee wengine na msemaji aliyitwa Tertulo, wakamsuta Paulo mbele ya mtawala nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baada ya siku tano, Anania, Kuhani Mkuu, akatelemka na baadhi ya wazee pamoja naye, na msemi mmoja, Tertulo, nao wakamweleza liwali habari za Paulo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulipopita siku tano, Kuhani Mukubwa Anania akaenda Kaisaria pamoja na wasimamizi wamoja wa watu na mutetezi mumoja wa sheria aliyeitwa Tertulo. Nao wakafika mbele ya liwali Feliki kwa kumushitaki Paulo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
BAADA ya siku tano, Anania, kuhani mkuu, akatelemka na baadhi ya wazee pamoja nae, na msemi mmoja, Tertullo nao wakamweleza liwali khabari za Paolo.