Acts 24:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ninachokubali mbele yako ni hiki: Mimi ninamwabudu Mungu wa wazee wetu nikiishi kufuatana na njia ile ambayo wao wanaiita chama cha uzushi. Ninaamini mambo yote yaliyoandikwa katika vitabu vya sheria na manabii.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ninakubali kwamba mimi namwabudu Mungu wa baba zetu kama mfuasi wa Njia Ile, ambayo wao wanaiita dhehebu. Ninaamini kila kitu kinachokubaliana na Torati na kile kilichoandikwa katika Manabii,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ila neno hili naungama kwako ya kwamba kwa Njia ile ambayo waiita uzushi, ndivyo ninavyomwabudu Mungu wa baba zetu, nikiyaamini yote yanayopatana na torati na yaliyoandikwa katika vyuo vya manabii.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini nitakuambia hili: Ninamuabudu Mungu, Mungu yule yule aliyeabudiwa na baba zetu, na kama mfuasi wa Njia, ambayo wayahudi hawa wanasema si njia sahihi. Na ninaamini kila kitu kinachofundishwa katika Sheria ya Musa na yote yaliyoandikwa katika vitabu vya manabii.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninachokubali mbele yako ni hiki: Mimi ninamwabudu Mungu na wazee wetu nikiishi kufuatana na Njia ile ambayo wao wanaiita chama cha uzushi. Ninaamini mambo yote yaliyoandikwa katika vitabu vya Sheria na manabii.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ninachokubali mbele yako ni hiki: Mimi ninamwabudu Mungu wa wazee wetu nikiishi kufuatana na njia ile ambayo wao wanaiita chama cha uzushi. Ninaamini mambo yote yaliyoandikwa katika vitabu vya sheria na manabii.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini, ninakubali kwamba mimi namwabudu Mungu wa baba zetu, mfuasi wa Njia, ile ambayo wao wanaiita dhehebu. Ninaamini kila kitu kinachokubaliana na Sheria na kile kilichoandikwa katika Manabii,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini, ninakubali kwamba mimi namwabudu Mungu wa baba zetu, mfuasi wa Njia, ile ambayo wao wanaiita dhehebu. Ninaamini kila kitu kinachokubaliana na Torati na kile kilichoandikwa katika Manabii,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ila neno hili naungama kwako ya kwamba kwa Njia ile ambayo waiita uzushi, ndivyo ninavyomwabudu Mungu wa baba zetu, nikiyaamini yote yanayopatana na torati na yaliyoandikwa katika vyuo vya manabii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ninachokubali mbele yako ni hiki: Mimi ninamwabudu Mungu wa wazee wetu nikiishi kufuatana na njia ile ambayo wao wanaiita chama cha uzushi. Ninaamini mambo yote yaliyoandikwa katika vitabu vya sheria na manabii.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mbele yako naungama waziwazi: Njia ile, wanayoiita ya chama, ndiyo yangu ya kumtumikia Mungu wa baba zetu, nikayategemea yote yaliyoandikwa penye Maonyo na katika vyuo vya Wafumbuaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ila neno hili naungama kwako ya kwamba kwa Njia ile ambayo waiita uzushi, ndivyo ninavyomwabudu Mungu wa baba zetu, nikiyaamini yote yanayopatana na torati na yaliyoandikwa katika vyuo vya manabii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ninakubali mbele yako kwamba ninamutumikia Mungu wa babu zetu nikifuata Njia ile wanayosema kwamba ni ya uongo. Mimi ninaamini maneno yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Sheria na katika vitabu vya manabii.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Illa neno hili naliungama kwako ya kwamba kwa Njia ile ambayo waiita uzushi, ndivyo ninavyomwabudu Mungu wa baba zetu, nikiyaamini yote yanayopatana na torati na yaliyoandikwa katika vyuo vya manabii.