Acts 24:18 — Compare Translations
13 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati nilipokuwa nikifanya hayo ndipo waliponikuta hekaluni, nilipokuwa nimekwisha fanya ile ibada ya kujitakasa. Hakukuwako kundi la watu wala ghasia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilikuwa nimetakaswa waliponikuta Hekaluni nikifanya mambo haya. Hapakuwa na umati wa watu pamoja nami, wala sikuhusika katika ghasia yoyote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaniona ndani ya hekalu nikishughulika na mambo haya, hali nimetakaswa, wala sikuwa na mkutano wala ghasia; lakini walikuwako baadhi ya Wayahudi waliotoka Asia,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati nilipokuwa nikifanya hayo ndipo waliponikuta Hekaluni, nilipokuwa nimekwisha fanya ile ibada ya kujitakasa. Hakukuwako kundi la watu wala ghasia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati nilipokuwa nikifanya hayo ndipo waliponikuta hekaluni, nilipokuwa nimekwisha fanya ile ibada ya kujitakasa. Hakukuwako kundi la watu wala ghasia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilikuwa nimeshatakaswa kwa taratibu za kiibada waliponikuta Hekaluni nikifanya mambo haya. Hapakuwa na umati wa watu, pamoja nami wala aliyehusika kwenye fujo yo yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilikuwa nimeshatakaswa kwa taratibu za kiibada waliponikuta Hekaluni nikifanya mambo haya. Hapakuwa na umati wa watu, pamoja nami wala aliyehusika kwenye fujo yoyote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaniona ndani ya hekalu nikishughulika na mambo haya, nilikuwa nimetakaswa, wala sikuwa na mkutano wala ghasia; lakini walikuwako baadhi ya Wayahudi waliotoka Asia,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati nilipokuwa nikifanya hayo ndipo waliponikuta hekaluni, nilipokuwa nimekwisha fanya ile ibada ya kujitakasa. Hakukuwako kundi la watu wala ghasia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo ndipo, waliponiona, nikieuliwa Patakatifu; hawakuniona, nikikusanya watu au nikipiga kelele.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaniona ndani ya hekalu nikishughulika na mambo haya, hali nimetakaswa, wala sikuwa na mkutano wala ghasia; lakini walikuwako baadhi ya Wayahudi waliotoka Asia,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na wakati ule nilipokuwa nikifanya mambo hayo, walinikuta katika hekalu, nami nilikuwa nimekwisha kufanya ibada ya kutakaswa. Sikukuwa na kundi la watu wala kuleta fujo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Baadhi ya Wayahudi waliotoka Asia wakaniona ndani ya hekalu nikishughulika na mambo haya, nimetakaswa, wala sikuwa pamoja na mkutano wala ghasia.