Acts 24:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kulikuwa na Wayahudi wengine kutoka mkoa wa Asia; hao ndio wangepaswa kuwa hapa mbele yako na kutoa mashtaka yao kama wana chochote cha kusema dhidi yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kuna Wayahudi fulani kutoka jimbo la Asia ambao walipaswa kuwa hapa mbele yako na kunishtaki kama wana jambo lolote dhidi yangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ambao imewapasa hao kuwapo hapa mbele yako na kunishitaki, kama wana neno lo lote juu yangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini baadhi ya Wayahudi kutoka Asia walikuwa pale. Walipaswa kuwa hapa mbele yako wakinishtaki ikiwa wana ushahidi kuwa nilifanya kitu chochote kibaya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini kulikuwa na Wayahudi wengine kutoka mkoa wa Asia; hao ndio wangepaswa kuwa hapa mbele yako na kutoa mashtaka yao kama wana chochote cha kusema dhidi yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kulikuwa na Wayahudi wengine kutoka mkoa wa Asia; hao ndio wangepaswa kuwa hapa mbele yako na kutoa mashtaka yao kama wana chochote cha kusema dhidi yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kulikuwa na baadhi ya Wayahudi kutoka Asia, ambao wangelazimika wawepo hapa mbele yako ili watoe mashtaka kama wanalo jambo lo lote dhidi yangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kulikuwa na baadhi ya Wayahudi kutoka Asia, ambao wangelazimika wawepo hapa mbele yako ili watoe mashtaka kama wanalo jambo lolote dhidi yangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ambao imewapasa hao kuwapo hapa mbele yako na kunishitaki, kama wana neno lolote juu yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kulikuwa na Wayahudi wengine kutoka mkoa wa Asia; hao ndio wangepaswa kuwa hapa mbele yako na kutoa mashtaka yao kama wana chochote cha kusema dhidi yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini walioniona ndio Wayuda wengine waliotoka Asia; hao ingewapasa kuwapo hapa, wanisute mbele yako, waliyonionea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ambao imewapasa hao kuwapo hapa mbele yako na kunishitaki, kama wana neno lo lote juu yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Wayuda wamoja waliotoka katika jimbo la Azia walikuwa pale, na ni hao ndio wangepaswa kuja mbele yako kunishitaki ikiwa wako na neno lolote juu yangu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Imewapasa hao kuwapo hapa mbele yako na kunishitaki kama wana neno lo lote juu yangu.