Acts 24:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Paulo aliitwa, na Tertulo akafungua mashtaka hivi: “Mheshimiwa Felisi, uongozi wako bora umeleta amani kubwa na marekebisho ya lazima yanafanywa kwa manufaa ya taifa letu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Paulo alipoitwa aingie ndani, Tertulo akaanza kutoa mashtaka akisema, “Mtukufu Feliksi, kwa muda mrefu tumefurahia amani na mabadiliko mengi mazuri yamefanywa kwa ajili ya watu hawa kwa sababu ya upeo wako wa kuona mambo ya mbele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alipoitwa, Tertulo akaanza kumshitaki, akisema, Kwa kuwa mnapata amani nyingi chini yako, Feliki mtukufu, na kwa maangalizi yako mambo mabaya yanatengenezwa kwa ajili ya taifa hili,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Paulo aliitwa kwenye mkutano, na Tertulo akaanza kueleza mashitaka. Tertulo alisema, “Mheshimiwa Feliki, kwa muda mrefu watu wetu wamefurahia amani kwa sababu yako, na mambo mengi mabaya katika nchi yetu yanarekebishwa kutokana na msaada wako wa hekima. Kwa hili sisi sote tunaendelea kushukuru.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Paulo aliitwa na Tertulo akafungua mashtaka hivi: “Mheshimiwa Felisi, uongozi wako bora umeleta amani kubwa na marekebisho ya lazima yanafanywa kwa manufaa ya taifa letu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Paulo aliitwa, na Tertulo akafungua mashtaka hivi: “Mheshimiwa Felisi, uongozi wako bora umeleta amani kubwa na marekebisho ya lazima yanafanywa kwa manufaa ya taifa letu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Paulo alipoitwa aingie ndani, Tertulo akaanza kutoa mashtaka akisema, “Mtukufu Feliksi, kwa muda mrefu tumefurahia amani na matengenezo mengi mazuri yamefanywa kwa ajili ya watu hawa kwa sababu ya upeo wako wa kuona mambo ya mbele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Paulo alipoitwa aingie ndani, Tertulo akaanza kutoa mashtaka akisema, “Mtukufu Feliksi, kwa muda mrefu tumefurahia amani na matengenezo mengi mazuri yamefanywa kwa ajili ya watu hawa kwa sababu ya upeo wako wa kuona mambo ya mbele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alipoitwa, Tertulo akaanza kumshitaki, akisema, Kwa kuwa mnapata amani nyingi chini yako, Feliki mtukufu, na kwa uongozi wako mambo mabaya yanasuluhishwa kwa ajili ya taifa hili,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Paulo aliitwa, na Tertulo akafungua mashtaka hivi: “Mheshimiwa Felisi, uongozi wako bora umeleta amani kubwa na marekebisho ya lazima yanafanywa kwa manufaa ya taifa letu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule alipoitwa, Tertulo akaanza kumsuta akisema: Kwa nguvu yako, bwana Feliki, tunapata kutengemana sana; na kwa utunzaji wako wewe hili taifa letu limetengenezewa mambo mazuri mengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alipoitwa, Tertulo akaanza kumshitaki, akisema, Kwa kuwa mnapata amani nyingi chini yako, Feliki mtukufu, na kwa maangalizi yako mambo mabaya yanatengenezwa kwa ajili ya taifa hili,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipomwita Paulo, Tertulo akaanza kumushitaki, akisema: “Muheshimiwa Feliki, kwa njia yako tumepata amani ya kweli. Na kwa uongozi wako umeleta mabadiliko mengi mazuri kwa ajili ya taifa hili.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na alipoitwa Tertullo akaanza kumshitaki, akisema,