Acts 24:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, Felisi, ambaye mwenyewe alikuwa anaifahamu hiyo njia vizuri, aliahirisha kesi hiyo. Akawaambia, “Nitatoa hukumu juu ya kesi hiyo wakati Lusia, mkuu wa jeshi, atakapokuja hapa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Feliksi, ambaye alifahamu vizuri habari za Njia Ile, akaahirisha kesi ile, akasema, “Jemadari Lisia atakapoteremka huku, nitaamua kesi yenu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Feliki aliwaahirisha, kwa sababu alijua habari za Njia ile kwa usahihi zaidi, akasema, Lisia jemadari atakapotelemka nitakata maneno yenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Feliki tayari alikuwa anaelewa mengi kuhusu Njia. Akasimamisha kesi na kusema, “Kamanda Lisiasi atakapokuja hapa, nitaamua nini cha kufanya.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo, Felisi, ambaye mwenyewe alikuwa anaifahamu hiyo Njia vizuri, aliahirisha kesi hiyo. Akawaambia, “Nitatoa hukumu juu ya kesi hiyo wakati Luisa, mkuu wa jeshi, atakapokuja hapa.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, Felisi, ambaye mwenyewe alikuwa anaifahamu hiyo njia vizuri, aliahirisha kesi hiyo. Akawaambia, “Nitatoa hukumu juu ya kesi hiyo wakati Lusia, mkuu wa jeshi, atakapokuja hapa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Feliksi ambaye alikuwa anafahamu vizuri habari za Njia ile, akaahirisha shauri lile kwa maelezo yake akisema, “Wakati jemadari Lisia atakapotelemka huku, nitaamua shauri lako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Feliksi ambaye alikuwa anafahamu vizuri habari za Njia ile, akaahirisha shauri lile kwa maelezo yake akisema, “Wakati jemadari Lisia atakapoteremka huku, nitaamua shauri lako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Feliki aliwaahirisha, kwa sababu alijua habari za Njia ile kwa usahihi zaidi, akasema, Lisia jemadari atakapoteremka nitaamua kesi yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo, Felisi, ambaye mwenyewe alikuwa anaifahamu hiyo njia vizuri, aliahirisha kesi hiyo. Akawaambia, “Nitatoa hukumu juu ya kesi hiyo wakati Lusia, mkuu wa jeshi, atakapokuja hapa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Feliki alipoyasikia haya akawakawilisha, kwani alipata kuelewa na mambo ya njia hiyo. Kwa hiyo akasema: Mkuu wa kikosi Lisia atakapotelemka, nitayatambulisha naye mambo yenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Feliki aliwaahirisha, kwa sababu alijua habari za Njia ile kwa usahihi zaidi, akasema, Lisia jemadari atakapotelemka nitakata maneno yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Feliki, aliyekuwa akifahamu vizuri mambo yanayoelekea Njia ya Bwana, akaamuru maneno yale yarudiliwe, akisema: “Nitakata maneno yenu wakati jemadari Lusia atakapokuja.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi Feliki, alijiokwisha kusikia haya, aliwaakhirisha, kwa sababu alijua khabari za Njia ile kwa usahihi zaidi, akasema, Lusia jemadari, atakapotelemka nitakata maneno yenu.