Acts 24:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akamwamuru yule jemadari amweke Paulo kizuizini, lakini awe na uhuru kiasi, na rafiki zake wasizuiwe kumpatia mahitaji yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo akaamuru kiongozi wa askari amweke chini ya ulinzi lakini ampe uhuru na kuwaruhusu rafiki zake wamhudumie.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwamuru yule akida kwamba Paulo alindwe; ila awe na nafasi, wala asimkataze mmojawapo wa rafiki zake kumtumikia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Feliki alimwambia ofisa wa jeshi kumlinda Paulo lakini wampe uhuru kiasi na wawaruhusu rafiki zake wamletee chochote atakachohitaji.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha akamwamuru yule jemadari amweke Paulo kizuizini, lakini awe na uhuru kiasi, na rafiki zake wasizuiwe kumpatia mahitaji yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akamwamuru yule jemadari amweke Paulo kizuizini, lakini awe na uhuru kiasi, na rafiki zake wasizuiwe kumpatia mahitaji yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo akaamuru mkuu wa maaskari amweke chini ya ulinzi lakini ampe uhuru na kuwaruhusu rafiki zake wamhudumie.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo akaamuru kiongozi wa askari amweke chini ya ulinzi lakini ampe uhuru na kuwaruhusu rafiki zake wamhudumie.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwamuru yule ofisa kwamba Paulo alindwe; ila awe na nafasi, wala asimkataze mmojawapo wa rafiki zake kumtumikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akamwamuru yule jemadari amweke Paulo kizuizini, lakini awe na uhuru kiasi, na rafiki zake wasizuiwe kumpatia mahitaji yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamwagiza bwana askari, Paulo alindwe, lakini asifungwe, wala asiwazuie wenziwe kumtumikia au kumjia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwamuru yule akida kwamba Paulo alindwe; ila awe na nafasi, wala asimkataze mmojawapo wa rafiki zake kumtumikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akamwamuru yule mukubwa wa jeshi kwamba wamulinde Paulo katika kifungo wakimwachia uhuru kidogo, na wasiwazuize warafiki zake kumusaidia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akamwamuru yule akida amlinde Paolo; illa awe na nafasi, wala asimkataze mmojawapo wa rafiki zake kumkhudumu au kuja kumtazama.