Acts 24:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tumegundua kwamba mtu huyu ni wa hatari mno. Yeye huanzisha ghasia kati ya Wayahudi kila mahali duniani na pia ni kiongozi wa kile chama cha Wanazareti.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Tumemwona mtu huyu kuwa ni msumbufu, anayechochea ghasia miongoni mwa Wayahudi duniani pote. Yeye ndiye kiongozi wa dhehebu la Wanasiri,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana tumemwona mtu huyu mkorofi, mwanzilishi wa fitina katika Wayahudi wote duniani, tena ni kichwa cha madhehebu ya Wanazorayo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtu huyu ni mkorofi. Anasababisha vurugu kwa Wayahudi kila mahali ulimwenguni. Ni kiongozi wa kundi la Wanazorayo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tumegundua kwamba mtu huyu ni wa hatari mno. Yeye huanzisha ghasia kati ya Wayahudi kila mahali duniani na pia ni kiongozi wa kile chama cha Wanazareti.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tumegundua kwamba mtu huyu ni wa hatari mno. Yeye huanzisha ghasia kati ya Wayahudi kila mahali duniani na pia ni kiongozi wa kile chama cha Wanazareti.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Tumemwona mtu huyu kuwa ni msumbufu, anayechochea ghasia miongoni mwa Wayahudi duniani pote. Yeye ndiye kiongozi wa dhehebu la Wanazarayo,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Tumemwona mtu huyu kuwa ni msumbufu, anayechochea ghasia miongoni mwa Wayahudi duniani pote. Yeye ndiye kiongozi wa dhehebu la Wanasiri,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana tumemwona mtu huyu kuwa mkorofi, mwanzilishi wa fitina katika Wayahudi wote duniani, tena ni kichwa cha madhehebu ya Wanazareti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tumegundua kwamba mtu huyu ni wa hatari mno. Yeye huanzisha ghasia kati ya Wayahudi kila mahali duniani na pia ni kiongozi wa kile chama cha Wanazareti.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani tumemwona mtu huyu kuwa mwangamizi, akiwaletea kondo Wayuda wote waliopo ulimwenguni po pote, tena ni mkubwa wa chama cha Wanasareti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana tumemwona mtu huyu mkorofi, mwanzilishi wa fitina katika Wayahudi wote duniani, tena ni kichwa cha madhehebu ya Wanazorayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tumetambua kwamba mutu huyu ni wa hatari sana, ameanzisha fujo kati ya Wayuda wote katika dunia. Tena yeye ni mukubwa wa chama cha Wanazareti.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana tamemwona mtu huyu mkorofi, muanzishaji wa fitina katika Mayahudi waliomo duniani, tena ni kichwa cha uzushi wa Wanazorayo.