Acts 25:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, ikiwa nimepatikana na kosa linalostahili adhabu ya kifo, siombi kusamehewa adhabu hiyo. Lakini kama hakuna ukweli katika mashtaka waliyotoa watu hawa, hakuna awezaye kunikabidhi kwao. Nakata rufani kwa Kaisari!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi kama mimi nina hatia ya kutenda kosa lolote linalostahili kifo, sikatai kufa. Lakini kama mashtaka yaliyoletwa dhidi yangu na hawa Wayahudi si kweli, hakuna yeyote aliye na haki ya kunikabidhi mikononi mwao. Naomba rufaa kwa Kaisari!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ikiwa ni mkosa au nimetenda neno la kustahili kufa, sikatai kufa; bali, kama si kweli neno hili wanalonishitaki, hapana awezaye kunitia mikononi mwao. Nataka rufani kwa Kaisari.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa nilitenda chochote kibaya na sheria inasema ni lazima nife, basi ninakubali kuwa ninapaswa kufa. Siombi kuokolewa kutokana na kifo. Lakini kama mashitaka haya siyo ya kweli, basi hakuna anayeweza kunikabidhi kwa watu hawa. Hapana, Nataka Kaisari aisikilize kesi yangu!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, ikiwa nimepatikana na kosa linalostahili adhabu ya kifo, siombi kusamehewa adhabu hiyo. Lakini kama hakuna ukweli katika mashtaka waliyotoa watu hawa, hakuna awezaye kunikabidhi kwao. Nakata rufani kwa Kaisari!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, ikiwa nimepatikana na kosa linalostahili adhabu ya kifo, siombi kusamehewa adhabu hiyo. Lakini kama hakuna ukweli katika mashtaka waliyotoa watu hawa, hakuna awezaye kunikabidhi kwao. Nakata rufani kwa Kaisari!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi kama mimi nina hatia ya kutenda kosa lo lote linalostahili kifo, sikatai kufa. Lakini kama mashtaka yaliyoletwa dhidi yangu na hawa Wayahudi si kweli, hakuna ye yote aliye na haki ya kunikabidhi mikononi mwao. Naomba rufaa kwa Kaisari!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi kama mimi nina hatia ya kutenda kosa lolote linalostahili kifo, sikatai kufa. Lakini kama mashtaka yaliyoletwa dhidi yangu na hawa Wayahudi si kweli, hakuna yeyote aliye na haki ya kunikabidhi mikononi mwao. Naomba rufaa kwa Kaisari!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ikiwa ni mkosa au nimetenda neno la kustahili kufa, sikatai kufa; bali, kama si kweli neno hili wanalonishitaki, hapana awezaye kunitia mikononi mwao. Nataka rufani kwa Kaisari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, ikiwa nimepatikana na kosa linalostahili adhabu ya kifo, siombi kusamehewa adhabu hiyo. Lakini kama hakuna ukweli katika mashtaka waliyotoa watu hawa, hakuna awezaye kunikabidhi kwao. Nakata rufani kwa Kaisari!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, nikiwa mpotovu, nikatenda linalopasa kuuawa, sikatai kufa. Lakini masingizio yao hawa yakiwa hayana maana, hakuna tena anayeweza kunitia mikononi mwao, kwamba awapendeze. Nataka, nihukumiwe na Kaisari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ikiwa ni mkosa au nimetenda neno la kustahili kufa, sikatai kufa; bali, kama si kweli neno hili wanalonishitaki, hapana awezaye kunitia mikononi mwao. Nataka rufani kwa Kaisari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mimi ni mukosaji au nimefanya kitendo kinachonipasa kuuawa, mimi sikatai kufa. Lakini kama hakuna ukweli wowote katika mashitaki yao juu yangu, hakuna mutu anayeweza kunitoa kwao. Ninaomba kusambishwa na Mufalme wa Roma.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ikiwa nimekosa au nimetenda neno la kustahili kufa, sikatai kufa; hali, kama si kweli neno hili wanalonishitaki, hapana awezae kunitia mikononi mwao. Nataka rufaani kwa Kaisari.