Acts 25:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ila tu walikuwa na mabishano kadhaa pamoja naye kuhusu dini yao na kuhusu mtu mmoja aitwaye Yesu ambaye alikufa, lakini Paulo anashikilia kwamba yu hai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Badala yake walikuwa na vipengele fulani vya kutokukubaliana naye kuhusu dini yao na kuhusu mtu aitwaye Isa aliyekufa, lakini Paulo alidai kwamba yu hai.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
bali walikuwa na maswali mengine mengine juu yake katika dini yao wenyewe, na katika habari ya mtu mmoja Yesu, aliyekuwa amekwisha kufa, ambaye Paulo alikaza kusema kwamba yu hai.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mashitaka yao yote yalihusu dini yao wenyewe na kuhusu mtu anayeitwa Yesu. Yesu alikufa lakini Paulo anasema bado yuko hai.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ila tu walikuwa na mabishano kadhaa pamoja naye kuhusu dini yao na kuhusu mtu mmoja aitwaye Yesu ambaye alikufa, lakini Paulo anashikilia kwamba yu hai.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ila tu walikuwa na mabishano kadhaa pamoja naye kuhusu dini yao na kuhusu mtu mmoja aitwaye Yesu ambaye alikufa, lakini Paulo anashikilia kwamba yu hai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Badala yake walikuwa na vipengele fulani vya kutokukubaliana naye kuhusu dini yao na juu ya mtu mmoja aitwaye Yesu, ambaye alikufa, lakini yeye Paulo alidai kwamba yu hai.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Badala yake walikuwa na vipengele fulani vya kutokukubaliana naye kuhusu dini yao na juu ya mtu mmoja aitwaye Isa, ambaye alikufa, lakini yeye Paulo alidai kwamba yu hai.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
bali walikuwa na maswali tofauti tofauti juu yake katika dini yao wenyewe, na kuhusu mtu mmoja Yesu, aliyekuwa amekwisha kufa, ambaye Paulo alikazania kusema kuwa yuko hai.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ila tu walikuwa na mabishano kadhaa pamoja naye kuhusu dini yao na kuhusu mtu mmoja aitwaye Yesu ambaye alikufa, lakini Paulo anashikilia kwamba yu hai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakabishana naye tu kwa ajili ya tambiko lao wenyewe na kwa ajili ya mfu anayeitwa Yesu, kwani Paulo alisema: Yupo, anaishi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
bali walikuwa na maswali mengine mengine juu yake katika dini yao wenyewe, na katika habari ya mtu mmoja Yesu, aliyekuwa amekwisha kufa, ambaye Paulo alikaza kusema kwamba yu hai.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walikuwa tu wakibishana naye juu ya dini yao wenyewe na juu ya mutu mumoja aliyeitwa Yesu; lakini Paulo alidai kwamba yuko muzima.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
hali walikuwa na maswali juu yake katika dini yao wenyewe, na katika khabari ya mtu mmoja Yesu, aliyekuwa amekwisha kufa, ambae Paolo alishika kusema kwamba yu hayi.