Acts 25:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Paulo alikata rufani, akaomba aachwe kizuizini mpaka uamuzi wa shauri hilo ufanywe na Kaisari. Kwa hiyo niliamua akae kizuizini mpaka nitakapoweza kumpeleka kwa Kaisari.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Paulo alipoomba afadhiliwe ili rufaa yake isikilizwe na Mfalme Agusto, nilimwamuru alindwe hadi nitakapoweza kumpeleka kwa Kaisari.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Paulo alipodai kuwekwa ahukumiwe na Kaisari, nikaamuru alindwe hata nitakapompeleka kwa Kaisari.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Paulo aliomba abaki mahabusu hapa Kaisaria. Anataka uamuzi kutoka kwa mfalme mkuu. Hivyo niliamua aendelee kushikiliwa hapa mpaka nitakapompeleka kwa Kaisari huko Rumi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Paulo alikata rufani, akaomba aachwe kizuizini mpaka uamuzi wa shauri hilo ufanywe na Kaisari. Kwa hiyo niliamua akae kizuizini mpaka nitakapoweza kumpeleka kwa Kaisari.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Paulo alikata rufani, akaomba aachwe kizuizini mpaka uamuzi wa shauri hilo ufanywe na Kaisari. Kwa hiyo niliamua akae kizuizini mpaka nitakapoweza kumpeleka kwa Kaisari.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Paulo alipoomba afadhiliwe ili rufaa yake isikilizwe na Mfalme Agusto, nilimwamuru alindwe mpaka nitakapoweza kumpeleka kwa Kaisari.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Paulo alipoomba afadhiliwe ili rufaa yake isikilizwe na Mfalme Agusto, nilimwamuru alindwe mpaka nitakapoweza kumpeleka kwa Kaisari.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Paulo alipodai kuwekwa ahukumiwe na Kaisari, nikaamuru alindwe hata nitakapompeleka kwa Kaisari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Paulo alikata rufani, akaomba aachwe kizuizini mpaka uamuzi wa shauri hilo ufanywe na Kaisari. Kwa hiyo niliamua akae kizuizini mpaka nitakapoweza kumpeleka kwa Kaisari.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Paulo akasema waziwazi, ya kuwa anataka kuwekwa, mpaka ahukumiwe na mfalme aliye mkuu peke yake; kwa hiyo nikaagiza, awekwe, mpaka nitakapomtuma kwake Kaisari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Paulo alipodai kuwekwa ahukumiwe na Kaisari, nikaamuru alindwe hata nitakapompeleka kwa Kaisari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wakati Paulo alipoomba maneno yake yakatwe na Mufalme wa Roma, nikaamuru alindwe katika kifungo mpaka nitakapomutuma kwa Mufalme wa Roma.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini Paolo alipodai kuwekwa ahukumiwe na Augusto, nikaamuru alindwe hatta nitakapompeleka kwa Kaisari.