Acts 25:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kisha akasema, “Mfalme Agripa na wote mlioko hapa pamoja nasi! Hapa mbele yenu yuko mtu ambaye jumuiya yote ya Wayahudi hapa na kule Yerusalemu walinilalamikia wakipiga kelele kwamba hastahili kuishi tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Festo akasema, “Mfalme Agripa, nanyi nyote mlio hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu! Jumuiya yote ya Kiyahudi wamenilalamikia kuhusu mtu huyu huko Yerusalemu na hapa Kaisaria, wakipiga kelele kwamba hapaswi kuendelea kuishi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Festo akasema, Mfalme Agripa, na ninyi nyote mliopo hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu, ambaye jamii yote ya Wayahudi huko Yerusalemu na hapa pia wamenitaka niwasaidie, wakipiga kelele kwamba haimpasi kuishi zaidi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Festo akasema, “Mfalme Agripa nanyi nyote mliokusanyika hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu. Wayahudi wote, hapa na Yerusalemu wamelalamika kwangu juu yake. Wanapolalamika, wanapaza sauti zao wakisema kwamba anapaswa kuuawa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha akasema, “Mfalme Agripa na wote mlioko hapa pamoja nasi! Hapa mbele yenu yuko mtu ambaye jumuiya yote ya Wayahudi hapa na kule Yerusalemu walinilalamikia wakipiga kelele kwamba hastahili kuishi tena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kisha akasema, “Mfalme Agripa na wote mlioko hapa pamoja nasi! Hapa mbele yenu yuko mtu ambaye jumuiya yote ya Wayahudi hapa na kule Yerusalemu walinilalamikia wakipiga kelele kwamba hastahili kuishi tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Festo akasema, “Mfalme Agripa, nanyi nyote mlio hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu! Jumuiya yote ya Kiyahudi wamenilalamikia kuhusu mtu huyu huko Yerusalemu na hapa Kaisaria, wakipiga kelele kwamba haimpasi kuendelea kuishi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Festo akasema, “Mfalme Agripa, nanyi nyote mlio hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu! Jumuiya yote ya Kiyahudi wamenilalamikia kuhusu mtu huyu huko Yerusalemu na hapa Kaisaria, wakipiga kelele kwamba haimpasi kuendelea kuishi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Festo akasema, Mfalme Agripa, na ninyi nyote mliopo hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu, ambaye jamii yote ya Wayahudi huko Yerusalemu na hapa pia wamenitaka niwasaidie, wakipiga kelele kwamba haimpasi kuishi zaidi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kisha akasema, “Mfalme Agripa na wote mlioko hapa pamoja nasi! Hapa mbele yenu yuko mtu ambaye jumuiya yote ya Wayahudi hapa na kule Yerusalemu walinilalamikia wakipiga kelele kwamba hastahili kuishi tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Festo aliposema: Mfalme Agripa, nanyi waume nyote mliopo hapa pamoja nasi, mtazameni mtu huyu! Kwa ajili yake yeye kundi lote zima la Wayuda limenitokea huko Yerusalemu na hapa vilevile; wakanipigia makelele ya kwamba: Haifai kabisa, huyu akiwapo vivyo hivyo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Festo akasema, Mfalme Agripa, na ninyi nyote mliopo hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu, ambaye jamii yote ya Wayahudi huko Yerusalemu na hapa pia wamenitaka niwasaidie, wakipiga kelele kwamba haimpasi kuishi zaidi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Festo akasema: “Mufalme Agripa, na ninyi wote munaokuwa hapa pamoja nasi, munamwona mutu huyu Wayuda wote waliyemushitaki kwangu kule Yerusalema na hapa vilevile wakilalamika kwamba hastahili kuishi tena.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Festo akasema, Mfalme Agrippa, na ninyi nyote mliopo hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu, ambae jamii yote ya Wayahudi huku Yerusalemi na hapa pia wamenitaka niwasaidie, wakipiga kelele kwamba haimpasi kuzidi kuishi.