Acts 25:26 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa upande wangu sina habari kamili ambayo naweza kumwandikia Kaisari juu yake. Ndiyo maana nimemleta hapa mbele yenu na mbele yako mfalme Agripa, ili baada ya kumchunguza, niweze kuwa na la kuandika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mimi sina kitu maalum cha kumwandikia Bwana Mtukufu kumhusu mtu huyu. Hivyo basi, nimemleta mbele yenu ninyi nyote, hasa mbele yako, Mfalme Agripa, ili kutokana na matokeo ya uchunguzi huu, niweze kupata kitu cha kuandika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami katika habari yake sina neno la hakika la kumwandikia bwana. Kwa hiyo nimemleta hapa mbele yenu, hasa mbele yako wewe, mfalme Agripa, ili akiisha kuulizwa-ulizwa nipate neno la kuandika.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hata hivyo, sifahamu kwa hakika ni nini cha kumwandikia bwana wangu Kaisari kama sababu ya kumpeleka mtu huyu kwake. Hivo nimemleta mbele yenu ninyi nyote, hasa wewe, Mfalme Agripa. Ninatumaini kwamba utamwuliza maswali na kunipa kitu cha kumwandikia Kaisari.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa upande wangu sina habari kamili ambayo naweza kumwandikia Kaisari juu yake. Ndiyo maana nimemleta hapa mbele yenu na mbele yako mfalme Agripa, ili baada ya kumchunguza, niweze kuwa na la kuandika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa upande wangu sina habari kamili ambayo naweza kumwandikia Kaisari juu yake. Ndiyo maana nimemleta hapa mbele yenu na mbele yako mfalme Agripa, ili baada ya kumchunguza, niweze kuwa na la kuandika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mimi sina kitu maalum cha kumwandikia mtukufu kumhusu mtu huyu. Kwa hiyo nimemleta mbele yenu ninyi nyote, hasa mbele yako, wewe Mfalme Agripa, ili kutokana na matokeo ya uchunguzi huu, niweze kupata kitu cha kuandika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mimi sina kitu maalum cha kumwandikia Bwana Mtukufu kumhusu mtu huyu. Kwa hiyo nimemleta mbele yenu ninyi nyote, hasa mbele yako, Mfalme Agripa, ili kutokana na matokeo ya uchunguzi huu, niweze kupata kitu cha kuandika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami katika habari yake sina neno la hakika la kumwandikia bwana. Kwa hiyo nimemleta hapa mbele yenu, hasa mbele yako wewe, mfalme Agripa, ili akiisha kuhojiwa nipate neno la kuandika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa upande wangu sina habari kamili ambayo naweza kumwandikia Kaisari juu yake. Ndiyo maana nimemleta hapa mbele yenu na mbele yako mfalme Agripa, ili baada ya kumchunguza, niweze kuwa na la kuandika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini sinalo neno la kweli la kumwandikia bwana wangu la kwamba: Amekosa hivi na hivi. Kwa hiyo nimemleta mbele yenu, kwanza mbele yako wewe, mfalme Agripa, nipate la kuandika, mkiisha kuulizana naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami katika habari yake sina neno la hakika la kumwandikia bwana. Kwa hiyo nimemleta hapa mbele yenu, hasa mbele yako wewe, mfalme Agripa, ili akiisha kuulizwa-ulizwa nipate neno la kuandika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi sina maneno kamili ya kumwandikia Mufalme wa Roma juu yake. Ndiyo maana nimemuleta mbele yenu na zaidi mbele yako, wewe mufalme Agripa, kusudi kisha kumwuliza, nipate maneno ya kuandika.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nami sina neno la hakika la kumwandikia Bwana. Kwa hiyo nimemleta hapa mbele yenu, illi akiisha kuulizwa khabari zake, nipate neno la kuandika.