Acts 25:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati Paulo alipofika, Wayahudi waliokuwa wametoka Yerusalemu walimzunguka wakaanza kutoa mashtaka mengi mazitomazito ambayo hawakuweza kuthibitisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Paulo alipotokea, wale Wayahudi waliokuwa wameteremka toka Yerusalemu wakasimama wakiwa wamemzunguka, wakileta mashtaka mengi mazito dhidi yake ambayo hawakuweza kuyathibitisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipokuja, wale Wayahudi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasimama karibu yake wakaleta mashitaka mengi mazito juu yake, wasiyoweza kuyayakinisha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Paulo aliingia kwenye chumba na Wayahudi waliokuja kutoka Yerusalemu walisimama kumzunguka. Walileta mashitaka mengi mazito dhidi yake, lakini hawakuweza kuthibitisha chochote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati Paulo alipofika, Wayahudi waliokuwa wametoka Yerusalemu walimzunguka wakaanza kutoa mashtaka mengi mazitomazito ambayo hawakuweza kuthibitisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati Paulo alipofika, Wayahudi waliokuwa wametoka Yerusalemu walimzunguka wakaanza kutoa mashtaka mengi mazitomazito ambayo hawakuweza kuthibitisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Paulo alipotokea, wale Wayahudi waliokuwa wametelemka toka Yerusalemu wakasimama wakiwa wamemzunguka, wakileta mashtaka mengi mazito dhidi yake ambayo hawakuweza kuyathibitisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Paulo alipotokea, wale Wayahudi waliokuwa wameteremka toka Yerusalemu wakasimama wakiwa wamemzunguka, wakileta mashtaka mengi mazito dhidi yake ambayo hawakuweza kuyathibitisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipokuja, wale Wayahudi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasimama karibu naye wakaleta mashitaka mengi mazito juu yake, wasiyoweza kuyayakinisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati Paulo alipofika, Wayahudi waliokuwa wametoka Yerusalemu walimzunguka wakaanza kutoa mashtaka mengi mazitomazito ambayo hawakuweza kuthibitisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipofika, Wayuda waliotelemka toka Yerusalemu wakamsimamia pande zote, wakamsingizia mambo mengi yaliyokuwa magumu, wasiweze kuyaonyesha kuwa ya kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipokuja, wale Wayahudi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasimama karibu yake wakaleta mashitaka mengi mazito juu yake, wasiyoweza kuyayakinisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati Paulo alipofika, wale Wayuda waliotoka Yerusalema wakamuzunguka na kutoa mashitaki mengi mazito juu yake ambayo wao hawawezi kuhakikisha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Walipokuja Wayahudi walioshuka kutoka Yerusalemi wakasimama karibu yake wakaleta mashitaka mengi na mazito juu yake, wasiyoweza kuyathuhutisha.