Acts 26:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mambo hayo ndiyo niliyoyafanya huko Yerusalemu. Mimi binafsi, nikiwa nimepewa mamlaka kutoka kwa makuhani wakuu, nilipata kuwatia gerezani wengi wa watu wa Mungu. Nao walipohukumiwa kuuawa, nilipiga kura ya kukubali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nami hayo ndiyo niliyoyafanya huko Yerusalemu. Kwa mamlaka ya viongozi wa makuhani, niliwafunga watakatifu wengi gerezani, na walipokuwa wakiuawa nilipiga kura yangu kuunga mkono.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nami nikayafanya hayo Yerusalemu; niliwafunga wengi miongoni mwa watakatifu ndani ya magereza, nikiisha kupewa amri na wakuu wa makuhani; na walipouawa nalitoa idhini yangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na ndivyo nilivyofanya, kuanzia Yerusalemu. Viongozi wa makuhani walinipa mamlaka ya kuwaweka gerezani watu wa Mungu wengi. Na walipokuwa wanauawa nilikubali kuwa lilikuwa jambo zuri.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mambo hayo ndiyo niliyoyafanya huko Yerusalemu. Mimi binafsi, nikiwa nimepewa mamlaka kutoka kwa makuhani wakuu, nilipata kuwatia gerezani wengi wa watu wa Mungu. Nao walipohukumiwa kuuawa, nilipiga kura ya kukubali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mambo hayo ndiyo niliyoyafanya huko Yerusalemu. Mimi binafsi, nikiwa nimepewa mamlaka kutoka kwa makuhani wakuu, nilipata kuwatia gerezani wengi wa watu wa Mungu. Nao walipohukumiwa kuuawa, nilipiga kura ya kukubali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nami hayo ndiyo nilivyofanya huko Yerusalemu. Kwa mamlaka ya viongozi wa makuhani, niliwatia wengi wa watakatifu gerezani na walipokuwa wakiuawa, nilipiga kura yangu kuunga mkono.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nami hayo ndiyo niliyoyafanya huko Yerusalemu. Kwa mamlaka ya viongozi wa makuhani, niliwatia wengi wa watakatifu gerezani na walipokuwa wakiuawa, nilipiga kura yangu kuunga mkono.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nami nikayafanya hayo Yerusalemu; niliwafunga wengi miongoni mwa watakatifu ndani ya magereza, nikiisha kupewa amri na wakuu wa makuhani; na walipouawa nilitoa idhini yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mambo hayo ndiyo niliyoyafanya huko Yerusalemu. Mimi binafsi, nikiwa nimepewa mamlaka kutoka kwa makuhani wakuu, nilipata kuwatia gerezani wengi wa watu wa Mungu. Nao walipohukumiwa kuuawa, nilipiga kura ya kukubali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayo niliyafanya huko Yerusalemu; nilipopewa ruhusa na watambikaji wakuu nikawatia watakatifu wengi kifungoni, tena walipouawa, nami nikasaidia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nami nikayafanya hayo Yerusalemu; niliwafunga wengi miongoni mwa watakatifu ndani ya magereza, nikiisha kupewa amri na wakuu wa makuhani; na walipouawa nalitoa idhini yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na ni vile nilivyofanya katika Yerusalema. Nilipata mamlaka toka kwa wakubwa wa makuhani; nami nikawatia watu watakatifu wengi wa Mungu katika kifungo. Na wakati walipowaua mimi nilikubali kwamba wanastahili kuuawa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nikayafanya Yerusalemi: niliwafunga wengi miongoni mwa watakatifu ndani ya magereza, nikiisha kupewa amri na makuhani wakuu; na walipouawa nalitoa idhini yangu.