Acts 26:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mheshimiwa, wakati nilipokuwa njiani, saa sita mchana, niliona mwanga mkubwa kuliko wa jua ukiangaza kutoka mbinguni, ukanizunguka mimi na wale wasafiri wenzangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ilikuwa yapata adhuhuri, ee mfalme, nilipokuwa njiani, niliona nuru kutoka mbinguni iliyong’aa kuliko jua, ikatuangaza pande zote, mimi na wale niliokuwa pamoja nao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Mfalme, ndipo wakati wa adhuhuri njiani naliona nuru inatoka mbinguni ipitayo mwangaza wa jua, ikinimulikia mimi, na wale waliofuatana nami pande zote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nikiwa njiani, mchana, niliona mwanga kutoka mbinguni, unaong'aa kuliko jua. Uling'aa kunizunguka mimi pamoja na wale waliokuwa wanasafiri pamoja nami.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mheshimiwa, wakati nilipokuwa njiani, saa sita mchana, niliona mwanga mkubwa kuliko wa jua ukiangaza kutoka mbinguni, ukanizunguka mimi na wale wasafiri wenzangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mheshimiwa, wakati nilipokuwa njiani, saa sita mchana, niliona mwanga mkubwa kuliko wa jua ukiangaza kutoka mbinguni, ukanizunguka mimi na wale wasafiri wenzangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ilikuwa yapata adhuhuri, Ee Mfalme, nilipokuwa njiani, niliona nuru kutoka mbinguni kali kuliko jua, iking'aa kunizunguka pande zote mimi na wale niliokuwa pamoja nao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ilikuwa yapata adhuhuri, ee mfalme, nilipokuwa njiani, niliona nuru kutoka mbinguni kali kuliko jua, iking’aa kunizunguka pande zote mimi na wale niliokuwa pamoja nao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee Mfalme, ndipo wakati wa adhuhuri njiani niliona nuru inatoka mbinguni ipitayo mwangaza wa jua, ikinimulikia mimi, na wale waliofuatana nami pande zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mheshimiwa, wakati nilipokuwa njiani, saa sita mchana, niliona mwanga mkubwa kuliko wa jua ukiangaza kutoka mbinguni, ukanizunguka mimi na wale wasafiri wenzangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ilipokuwa saa sita ya mchana, ndipo, mfalme, nilipoona hapo njiani mwanga uliotoka mbinguni wenye kumetuka kulishinda jua, ukatumulikia pande zote mimi na wenzangu waliokwenda pamoja nami.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee Mfalme, ndipo wakati wa adhuhuri njiani naliona nuru inatoka mbinguni ipitayo mwangaza wa jua, ikinimulikia mimi, na wale waliofuatana nami pande zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ee mufalme, nilipokuwa katika njia, ilipotimia saa sita ya muchana, nikaona mwangaza unaotoka mbinguni unaopita mwangaza wa jua. Mwangaza ule ukanizunguka pamoja na wenzangu waliosafiri nami.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ee Mfalme, wakati wa adhdhuhuri njiani naliona nuru inatoka mbinguni ipitayo mwangaza wa jua, ikinimulikia mimi, na wale waliofuatana nami pande zote.