Acts 26:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sisi sote tulianguka chini, nami nikasikia sauti ikiniambia kwa Kiebrania: ‘Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa? Unajiumiza bure kama ng'ombe anayepiga teke fimbo ya bwana wake.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wote tulianguka chini, nami nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya Kiebrania, ‘Sauli, Sauli, mbona unanitesa? Ni vigumu kwako kuupiga teke mchokoo.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tukaanguka nchi sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya kiebrania, Sauli! Sauli! Mbona waniudhi? Ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sote tulianguka chini. Kisha nilisikia sauti iliyozungumza nami kwa Kiaramu. Sauti ilisema, ‘Sauli, Sauli, kwa nini unanitesa? Unajiumiza wewe mwenyewe kwa kunipinga mimi.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sisi sote tulianguka chini, nami nikasikia sauti ikiniambia kwa Kiebrania: Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa? Unajiumiza bure kama punda anayepiga teke fimbo ya bwana wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sisi sote tulianguka chini, nami nikasikia sauti ikiniambia kwa Kiebrania: ‘Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa? Unajiumiza bure kama ng'ombe anayepiga teke fimbo ya bwana wake.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wote tulipokuwa tumeanguka chini, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya Kiebrania, ‘Sauli, Sauli, mbona unanitesa? Ni vigumu kwako kuupiga teke mchokoo.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wote tulipokuwa tumeanguka chini, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya Kiebrania, ‘Sauli, Sauli, mbona unanitesa? Ni vigumu kwako kuupiga teke mchokoo.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tukaanguka chini sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya Kiebrania, Sauli! Sauli! Mbona waniudhi? Ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sisi sote tulianguka chini, nami nikasikia sauti ikiniambia kwa Kiebrania: ‘Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa? Unajiumiza bure kama ng'ombe anayepiga teke fimbo ya bwana wake.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tulipoanguka chini sote, nikasikia sauti iliyoniambia kwa msemo wa Kiebureo: Sauli, Sauli, unanifukuzaje? Utashindwa na kupiga mateke penye machomeo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tukaanguka nchi sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya kiebrania, Sauli! Sauli! Mbona waniudhi? Ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sisi wote tukaanguka chini, na nikasikia sauti iliyoniambia hivi katika luga ya Kiebrania: ‘Saulo, Saulo, kwa sababu gani unanitesa? Unajiumiza bure kama ngombe anayepiga teke kwenye chongo ya fimbo ya mwenyeji wake.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tukaanguka chini sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya Kiebrania, Saul! Saul! ya nini kunindhi? ni vigumu kwako kunpiga mateke mchokoo.