Acts 26:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Haidhuru, inuka sasa; simama wima. Nimekutokea ili nikuweke rasmi kuwa mtumishi wangu. Utawathibitishia watu wengine mambo uliyoyaona leo na yale ambayo bado nitakuonesha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa inuka usimame kwa miguu yako. Nimekutokea ili nikuteue uwe mtumishi na shahidi wa mambo ambayo umeyaona, na yale nitakayokuonesha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini inuka, usimame kwa miguu yako, maana nimekutokea kwa sababu hii, nikuweke wewe uwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Simama! Nimekuchagua wewe kuwa mtumishi wangu. Utawaambia watu habari zangu, ulichoona leo na yale nitakayokuonesha. Hii ndiyo sababu nimekuja kwako.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Haidhuru, inuka sasa; simama wima. Nimekutokea ili nikuweke rasmi kuwa mtumishi wangu. Utawathibitishia watu wengine mambo uliyoyaona leo na yale ambayo bado nitakuonyesha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Haidhuru, inuka sasa; simama wima. Nimekutokea ili nikuweke rasmi kuwa mtumishi wangu. Utawathibitishia watu wengine mambo uliyoyaona leo na yale ambayo bado nitakuonesha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini sasa inuka usimame kwa miguu yako, kwa sababu nimekutokea kwa kusudi hili, ili kukuweka utumike na kushuhudia juu ya mambo ambayo umeyaona na yale nitakayokutokea kwayo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa inuka usimame kwa miguu yako. Nimekutokea ili nikuteue uwe mtumishi na shahidi wa mambo ambayo umeyaona, na yale nitakayokuonyesha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini inuka, usimame kwa miguu yako, maana nimekutokea kwa sababu hii, nikuweke wewe uwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Haidhuru, inuka sasa; simama wima. Nimekutokea ili nikuweke rasmi kuwa mtumishi wangu. Utawathibitishia watu wengine mambo uliyoyaona leo na yale ambayo bado nitakuonesha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini inuka, usimame kwa miguu yako! Kwani hii ndiyo, niliyokutokea; Nikulinganye, utumike kuyashuhudia, uliyoyaona, nayo utakayoonyeshwa nami.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini inuka, usimame kwa miguu yako, maana nimekutokea kwa sababu hii, nikuweke wewe uwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sasa inuka usimame wima. Nimekutokea kusudi nikuweke kuwa mutumishi wangu. Wewe utatoa ushuhuda juu yangu; utawaelezea watu mambo uliyoona leo na yale nitakayokuonyesha nyuma.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini inuka, usimame, maana nimekutokea kwa sababu hii, nikuweke nwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo kwayo nitajidhihirisha kwako;