Acts 26:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
yaani ilimpasa Kristo ateseke na kuwa wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu, ili atangaze kwamba mwanga wa ukombozi unawaangazia sasa watu wote, Wayahudi na pia watu wa mataifa mengine.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwamba Al-Masihi atateswa, na kwamba yeye atakuwa wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu, na atatangaza nuru kwa watu wake na kwa watu wa Mataifa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ya kwamba Kristo hana budi kuteswa na ya kwamba yeye kwanza kwa kufufuliwa katika wafu atatangaza habari za nuru kwa watu wake na kwa watu wa Mataifa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walisema kwamba Masihi atakufa na kuwa wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu. Walisema kwamba ataleta mwanga wa kweli ya Mungu inayowaokoa wote, Wayahudi na wasio Wayahudi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
yaani ilimpasa Kristo ateseke na kuwa wa kwanza kufufuka kutoka wafu, ili atangaze kwamba mwanga wa ukombozi unawaangazia sasa watu wote, Wayahudi na pia watu wa mataifa mengine.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
yaani ilimpasa Kristo ateseke na kuwa wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu, ili atangaze kwamba mwanga wa ukombozi unawaangazia sasa watu wote, Wayahudi na pia watu wa mataifa mengine.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwamba Kristo atateswa na kwamba yeye atakuwa wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu, atatangaza nuru kwa watu wake na kwa watu Mataifa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwamba Al-Masihi atateswa, na kwamba yeye atakuwa wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu, na atatangaza nuru kwa watu wake na kwa watu wa Mataifa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ya kwamba Kristo hana budi kuteswa na ya kwamba yeye kwanza kwa kufufuliwa katika wafu atatangaza habari za nuru kwa watu wake na kwa watu wa Mataifa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
yaani ilimpasa Kristo ateseke na kuwa wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu, ili atangaze kwamba mwanga wa ukombozi unawaangazia sasa watu wote, Wayahudi na pia watu wa mataifa mengine.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatakayokuwapo ni haya: Kristo sharti ateswe, kisha atakuwa limbuko la ufufuko wa wafu, kisha atawaalika wao wa ukoo huu nao wamizimu, wafike mwangani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ya kwamba Kristo hana budi kuteswa na ya kwamba yeye kwanza kwa kufufuliwa katika wafu atatangaza habari za nuru kwa watu wake na kwa watu wa Mataifa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wao walitangaza kwamba Kristo anapaswa kuteswa na kuwa wa kwanza kufufuka kati ya wote waliokufa, naye atahubiri kwa Wayuda na kwa watu wa mataifa mengine kwamba kwa njia ya kuokolewa wataweza kuishi katika mwangaza.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ya kwamba Kristo hana buddi kuteswa na ya kwamba yeye kwanza kwa kufufuliwa katika wafu atatangaza khabari za nuru kwa watu wake na kwa watu wa mataifa.