Acts 26:29 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Paulo akamjibu, “Namwomba Mungu kwamba, kwa muda mfupi au mrefu, si wewe tu bali wote wanaonisikia leo wapate kuwa kama nilivyo mimi, lakini bila hii minyororo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Paulo akasema, “Ikiwa ni kwa haraka au la, namwomba Mungu, si wewe peke yako bali pia wale wote wanaonisikiliza leo, wawe kama mimi nilivyo, kasoro minyororo hii.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Paulo akamjibu, Namwomba Mungu kwamba, ikiwa kwa machache au ikiwa kwa mengi, si wewe tu ila na hao wote wanaonisikia leo wawe kama mimi, isipokuwa vifungo hivi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Paulo akasema, “Haijalishi kwangu, ikiwa ni vigumu au rahisi. Ninaomba tu kwa Mungu kwamba si wewe peke yako lakini kila mtu anayenisikiliza leo angeokolewa ili awe kama mimi, isipokuwa kwa minyororo hii!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Paulo akamjibu, “Namwomba Mungu kwamba, kwa muda mfupi au mrefu, si wewe tu bali wote wanaonisikia leo wapate kuwa kama nilivyo mimi, lakini bila hii minyororo.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Paulo akamjibu, “Namwomba Mungu kwamba, kwa muda mfupi au mrefu, si wewe tu bali wote wanaonisikia leo wapate kuwa kama nilivyo mimi, lakini bila hii minyororo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Paulo akasema, “Ikiwa ni kwa haraka au la, namwomba Mungu, si wewe peke yako bali pia wale wote wanaonisikiliza leo, wawe kama mimi nilivyo, isipokuwa minyororo hii.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Paulo akasema, “Ikiwa ni kwa haraka au la, namwomba Mungu, si wewe peke yako bali pia wale wote wanaonisikiliza leo, wawe kama mimi nilivyo, kasoro minyororo hii.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Paulo akamjibu, Namwomba Mungu kwamba, ikiwa kwa machache au ikiwa kwa mengi, si wewe tu ila na hao wote wanaonisikia leo wawe kama mimi, isipokuwa kuwa katika minyororo hii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Paulo akamjibu, “Namwomba Mungu kwamba, kwa muda mfupi au mrefu, si wewe tu bali wote wanaonisikia leo wapate kuwa kama nilivyo mimi, lakini bila hii minyororo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Paulo aliposema: Namwomba Mungu, paliposalia padogo napo paliposalia pakubwa, wote hapa walionisikia leo, si wewe tu, awape kuwa, kama mimi nilivyo, pasipo minyororo hii.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Paulo akamjibu, Namwomba Mungu kwamba, ikiwa kwa machache au ikiwa kwa mengi, si wewe tu ila na hao wote wanaonisikia leo wawe kama mimi, isipokuwa vifungo hivi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Paulo akajibu: “Ikiwa wakati kidogo au wakati murefu, ninamwomba Mungu, si juu yako wewe mwenyewe tu, lakini hata hawa wote wanaonisikiliza leo wapate kuwa sawa mimi, lakini wasifikie tu kutiwa katika kifungo!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Paolo akamjibu, Namwomba Mungu kwamba ikiwa kwa machache au ikiwa kwa mengi si wewe tu illa na hao wote wanaonisikia leo wawe kama mimi pasipo vifungo hivi.