Acts 26:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wananifahamu kwa muda mrefu, na wanaweza kushuhudia, kama wakipenda, kwamba tangu mwanzo niliishi kama mmoja wa kikundi chenye siasa kali kabisa katika dini yetu, yaani kikundi cha Mafarisayo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wao wamenifahamu kwa muda mrefu, na wanaweza kushuhudia wakipenda kushuhudia, kwamba kutokana na misimamo mikali sana ya dhehebu letu kwenye dini yetu, niliishi nikiwa Farisayo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakinijua sana tangu mwanzo, kama wakipenda kushuhudia, ya kwamba nalikuwa Farisayo kwa kuifuata madhehebu ya dini yetu iliyo sahihi kabisa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wayahudi hawa wamenifahamu kwa muda mrefu. Wakitaka wanaweza kukwambia kwamba nilikuwa Farisayo mzuri. Na Mafarisayo wanazitii sheria za dini ya Kiyahudi kwa uangalifu kuliko kundi lolote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wananifahamu kwa muda mrefu, na wanaweza kushuhudia, kama wakipenda, kwamba tangu mwanzo niliishi kama mmoja wa kikundi chenye siasa kali zaidi katika dini yetu, yaani kikundi cha Mafarisayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wananifahamu kwa muda mrefu, na wanaweza kushuhudia, kama wakipenda, kwamba tangu mwanzo niliishi kama mmoja wa kikundi chenye siasa kali kabisa katika dini yetu, yaani kikundi cha Mafarisayo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wao wamefahamu kwa muda mrefu na wanaweza kushuhudia kama wakipenda, kutokana na misimamo mikali sana ya dhehebu letu kwenye dini yetu niliishi nikiwa Farisayo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wao wamefahamu kwa muda mrefu na wanaweza kushuhudia kama wakipenda, ya kwamba kutokana na misimamo mikali sana ya dhehebu letu kwenye dini yetu, niliishi nikiwa Farisayo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakinijua sana tangu mwanzo, kama wakipenda kushuhudia, ya kwamba nilikuwa Farisayo kwa kuifuata madhehebu ya dini yetu iliyo sahihi kabisa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wananifahamu kwa muda mrefu, na wanaweza kushuhudia, kama wakipenda, kwamba tangu mwanzo niliishi kama mmoja wa kikundi chenye siasa kali kabisa katika dini yetu, yaani kikundi cha Mafarisayo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wamenitambua kale; wakitaka wangenishuhudia, ya kwamba nimekifuata kile chama kinachokaza kuyashika mambo ya tambiko letu, kwani nalikuwa Fariseo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakinijua sana tangu mwanzo, kama wakipenda kushuhudia, ya kwamba nalikuwa Farisayo kwa kuifuata madhehebu ya dini yetu iliyo sahihi kabisa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wamenijua tangu zamani na kama wakitaka wanaweza kushuhudia kwamba nilikuwa mushiriki wa chama cha Wafarisayo, kinachotia mukazo sana juu ya kushika desturi za dini yetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakinijua sana tangu mwanzo, kama wakipenda kushuhudia, ya kwamba nalikuwa Farisayo kwa kuifuata madhehebu ya dini yetu iliyo sahihi kabisa.