Acts 27:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipokwisha amua tusafiri mpaka Italia, walimweka Paulo pamoja na wafungwa wengine chini ya ulinzi wa Yulio aliyekuwa ofisa wa jeshi katika kikosi kiitwacho “Kikosi cha Augusto.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ilipoamuliwa kwamba tungesafiri kwa meli kwenda Italia, Paulo na wafungwa wengine wakakabidhiwa kwa kiongozi mmoja wa askari aliyeitwa Juliasi, aliyekuwa wa Kikosi cha Walinzi wa Kaisari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ilipoamriwa tuabiri hata Italia, wakamtia Paulo na wafungwa wengine katika mikono ya akida mmoja, jina lake Yulio, wa kikosi cha Augusto.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Iliamriwa kwamba tutakwenda Italia. Ofisa wa Jeshi aliyeitwa Yulio, aliyetumika katika jeshi maalumu la mfalme mkuu, aliwekwa kuwa kiongozi wa kumlinda Paulo na baadhi ya wafungwa wengine safarini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walipokwisha amua tusafiri mpaka Italia, walimweka Paulo pamoja na wafungwa wengine chini ya ulinzi wa Yulio aliyekuwa ofisa wa jeshi katika kikosi kiitwacho “Kikosi cha Augusto.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipokwisha amua tusafiri mpaka Italia, walimweka Paulo pamoja na wafungwa wengine chini ya ulinzi wa Yulio aliyekuwa ofisa wa jeshi katika kikosi kiitwacho “Kikosi cha Augusto.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ilipoamuliwa kwamba tungesafiri kwa njia ya bahari kwenda Italia, Paulo na wafungwa wengine wakakabidhiwa kwa askari mmoja jina lake Juliasi, ambaye alikuwa wa kikosi cha walinzi wa Kaisari Agusto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ilipoamuliwa kwamba tungesafiri kwa njia ya bahari kwenda Italia, Paulo na wafungwa wengine wakakabidhiwa kwa kiongozi mmoja wa askari aliyeitwa Juliasi, aliyekuwa wa Kikosi cha Walinzi wa Kaisari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ilipoamriwa tuabiri hadi Italia, wakamtia Paulo na wafungwa wengine katika mikono ya ofisa mmoja, jina lake Yulio, wa kikosi cha Augusto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipokwisha amua tusafiri mpaka Italia, walimweka Paulo pamoja na wafungwa wengine chini ya ulinzi wa Yulio aliyekuwa ofisa wa jeshi katika kikosi kiitwacho “Kikosi cha Augusto.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mambo yalipokatwa, kwamba tutweke kwenda Italia, wakamtia Paulo na wafungwa wengine mikononi mwa bwana askari, jina lake Yulio aliyekuwa wa kikosi kilichomlinda mfalme aliye mkuu peke yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ilipoamriwa tuabiri hata Italia, wakamtia Paulo na wafungwa wengine katika mikono ya akida mmoja, jina lake Yulio, wa kikosi cha Augusto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipokwisha kukamata mupango wa kutusafirisha kwa njia ya chombo mpaka Italia, wakamuweka Paulo na wafungwa wengine chini ya uangalizi wa mukubwa mumoja wa waaskari aliyeitwa Yulio. Yeye alikuwa wa kundi la waaskari lililoitwa “Kundi la waaskari wa mufalme.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
BASSI ilipoamriwa tusafiri hatta Italia, wakamtia Paolo na wafungwa wengine katika mikono ya akida mmoja, jina lake Yulio, wa kikosi cha Augusto.