Acts 27:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, upepo mzuri wa kusi ulianza kuvuma, nao wakadhani wamefanikiwa lengo lao; hivyo wakangoa nanga, wakaiendesha meli karibu sana na pwani ya Krete.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Upepo mtulivu ulipoanza kuvuma toka kusini, wakadhani kuwa wangeweza kufikia lengo lao, hivyo wakang’oa nanga na kusafiri wakipita kandokando ya pwani ya kisiwa cha Krete.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na upepo wa kusi ulipoanza kuvuma kidogo, wakidhani ya kuwa wamepata waliyoazimu kupata, wakang'oa nanga, wakasafiri karibu na Krete pwani kwa pwani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo upepo mzuri ukaanza kuvuma kutoka kusini. Watu ndani ya meli wakafikiri, “Huu ndio upepo tulioutaka, na sasa tumeupata!” Hivyo wakavuta nanga. Tulitweka tanga tukasafiri karibu na kisiwa cha Krete.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, upepo mzuri wa kusi ulianza kuvuma, nao wakadhani wamefanikiwa lengo lao; hivyo wakang'oa nanga, wakaiendesha meli karibu sana na pwani ya Krete.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, upepo mzuri wa kusi ulianza kuvuma, nao wakadhani wamefanikiwa lengo lao; hivyo wakang'oa nanga, wakaiendesha meli karibu sana na pwani ya Krete.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Upepo mtulivu ulipoanza kuvuma toka kusini, wakadhani kuwa wangeweza kufikia lengo lao, hivyo wakang'oa nanga na kusafiri wakipita kandokando ya pwani ya kisiwa cha Krete.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Upepo mtulivu ulipoanza kuvuma toka kusini, wakadhani kuwa wangeweza kufikia lengo lao, hivyo wakang’oa nanga na kusafiri wakipita kandokando ya pwani ya kisiwa cha Krete.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na upepo wa kusi ulipoanza kuvuma kidogo, wakidhani ya kuwa wamepata waliyoazimu kupata, wakang'oa nanga, wakasafiri karibu na Krete kandokando ya pwani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, upepo mzuri wa kusi ulianza kuvuma, nao wakadhani wamefanikiwa lengo lao; hivyo wakangoa nanga, wakaiendesha meli karibu sana na pwani ya Krete.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Upepo wa kusini ulipoanza kuvuma, wakawaza, ya kuwa wamavipata, walivyovitaka, wakang'oa nanga, wakaendelea kandokando ya pwani pa Kreta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na upepo wa kusi ulipoanza kuvuma kidogo, wakidhani ya kuwa wamepata waliyoazimu kupata, wakang’oa nanga, wakasafiri karibu na Krete pwani kwa pwani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Upepo usiokuwa mukali ulipoanza kuvuma tokea kusini, wakazani kwamba wataweza tu kutimiza sawa walivyokuwa wamekusudia. Wakapandisha nanga na kuendelea pembenipembeni karibu sana na Krete.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na upepo wa kusi ulipoanza kuvuma kidogo, wakidhani ya kuwa wamepata walioazimu kupata, wakangʼoa nanga, wakasafiri karibu na Krete pwani kwa pwani.