Acts 27:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisiwa kimoja kiitwacho Kauda kilitukinga kidogo na ule upepo; na tulipopita kusini mwake tulifaulu, ingawa kwa shida, kuusalimisha ule mtumbwi wa meli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hatimaye tukisafiri kupita chini ya kisiwa kidogo kiitwacho Kauda, ambapo kwa kuwa tulikuwa tumekingiwa upepo na hicho kisiwa, tuliweza kwa shida kuifunga mashua ya kuokolea watu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tukipita upesi karibu na kisiwa kidogo kiitwacho Kauda tukadiriki kuikweza mashua; lakini kwa shida.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tulikwenda upande wa chini wa kisiwa kidogo kilichoitwa Kauda. Kisiwa kikatukinga dhidi ya upepo, tulichukua mtumbwi wa kuokolea watu, lakini ilikuwa vigumu sana kufanya hivyo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisiwa kimoja kiitwacho Kanda kilitukinga kidogo na ule upepo; na tulipopita kusini mwake tulifaulu, ingawa kwa shida, kuusalimisha ule mtumbwi wa meli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisiwa kimoja kiitwacho Kauda kilitukinga kidogo na ule upepo; na tulipopita kusini mwake tulifaulu, ingawa kwa shida, kuusalimisha ule mtumbwi wa meli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hatimaye tukisafiri kupita chini ya kisiwa kidogo kiitwacho Kauda, ambapo kwa kuwa tulikuwa tumekingiwa upepo na hicho kisiwa, tuliweza kwa shida kuifunga mashua ya kuokolea watu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hatimaye tukisafiri kupita chini ya kisiwa kidogo kiitwacho Kauda, ambapo kwa kuwa tulikuwa tumekingiwa upepo na hicho kisiwa, tuliweza kwa shida kuifunga mashua ya kuokolea watu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tukipita upesi karibu na kisiwa kidogo kiitwacho Kauda tukadiriki kuikweza mashua; lakini kwa shida.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisiwa kimoja kiitwacho Kauda kilitukinga kidogo na ule upepo; na tulipopita kusini mwake tulifaulu, ingawa kwa shida, kuusalimisha ule mtumbwi wa meli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tukaenenda na kukimbizwa na upepo, tukafika kwenye kisiwa kidogo, jina lake Klauda, hapo tukakaza nguvu zote, tupate kuipandisha mashua; palisalia kidogo tu, tungeshindwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tukipita upesi karibu na kisiwa kidogo kiitwacho Kauda tukadiriki kuikweza mashua; lakini kwa shida.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tulipokuwa tukipita upande wa kusini wa kisanga kidogo kinachoitwa Kauda, tuliweza kwa shida sana kuopoa mutumbwi unaokokotwa na chombo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na tukipita upesi karibu na kisiwa kiitwacho Klaudia tukadiriki kuikweza mashua; kwa shidda lakini.