Acts 27:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa muda wa siku nyingi hatukuweza kuona jua wala nyota; dhoruba iliendelea kuvuma sana, hata matumaini yote ya kuokoka yakatuishia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati jua wala nyota hazikuonekana kwa siku nyingi, na dhoruba iliendelea kuvuma, hatimaye tulikata tamaa ya kuokolewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jua wala nyota hazikuonekana kwa muda wa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, basi tukakata tamaa ya kuokoka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa siku nyingi hatukuweza kuliona jua au nyota. Dhoruba ilikuwa mbaya sana. Tulipoteza matumaini yote ya kuendelea kuwa hai, tulidhani tutakufa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa muda wa siku nyingi hatukuweza kuona jua wala nyota; dhoruba iliendelea kuvuma sana, hata matumaini yote ya kuokoka yakatuishia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa muda wa siku nyingi hatukuweza kuona jua wala nyota; dhoruba iliendelea kuvuma sana, hata matumaini yote ya kuokoka yakatuishia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kulipokuwa hakuna kuonekana kwa jua wala nyota kwa siku nyingi, nayo dhoruba ikiwa inaendelea kuwa kali, hatimaye tulikata kabisa tamaa ya kuokoka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kulipokuwa hakuna kuonekana kwa jua wala nyota kwa siku nyingi, nayo dhoruba ikiwa inaendelea kuwa kali, hatimaye tulikata kabisa tamaa ya kuokoka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jua wala nyota hazikuonekana kwa muda wa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, basi tukakata tamaa ya kuokoka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa muda wa siku nyingi hatukuweza kuona jua wala nyota; dhoruba iliendelea kuvuma sana, hata matumaini yote ya kuokoka yakatuishia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakinia zilipokuwa siku nyingi, lisituonekee wala jua wala nyota, upepo ukikaza vivyo hivyo, basi, mwisho hakuwako tena mwenye moyo wa kwamba: Tutaokoka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jua wala nyota hazikuonekana kwa muda wa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, basi tukakata tamaa ya kuokoka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa muda wa siku nyingi hatukuweza kuona tena jua wala nyota, nayo zoruba ikaendelea kuvuma kwa nguvu. Kwa mwisho tukakata kitumaini chote cha kupona.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na jua na nyota hazikuonekana kwa muda wa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, bassi tukakata tamaa ya kuokoka.