Acts 27:27 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Usiku wa siku ya kumi na nne, tulikuwa tunakokotwa huku na huko katika bahari ya Adria. Karibu na usiku wa manane wanamaji walijihisi kuwa karibu na nchi kavu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Usiku wa kumi na nne ulipofika, tulikuwa bado tunasukumwa na upepo katika Bahari ya Adria. Ilipokuwa yapata usiku wa manane, mabaharia wakahisi kwamba walikuwa wanakaribia nchi kavu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata usiku wa kumi na nne ulipofika, tulipokuwa tukichukuliwa huko na huko katika bahari ya Adria, kama usiku wa manane baharia wakadhani ya kuwa wanaikaribia nchi kavu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Usiku wa kumi na nne tulikuwa bado tunasukumwa na upepo katika bahari ya Adriatiki. Mabaharia wakadhani tulikuwa karibu na nchi kavu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Usiku wa siku ya kumi na nne, tulikuwa tunakokotwa huku na huku katika bahari ya Adria. Karibu na usiku wa manane wanamaji walijihisi kuwa karibu na nchi kavu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Usiku wa siku ya kumi na nne, tulikuwa tunakokotwa huku na huko katika bahari ya Adria. Karibu na usiku wa manane wanamaji walijihisi kuwa karibu na nchi kavu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Usiku wa kumi na nne, ulipofika, tulipokuwa bado tunasukumwa na upepo katika Bahari ya Adria, ilipokuwa yapata usiku wa manane, mabaharia wakahisi kwamba walikuwa wanakaribia nchi kavu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Usiku wa kumi na nne ulipofika, tulikuwa bado tunasukumwa na upepo katika Bahari ya Adria. Ilipokuwa yapata usiku wa manane, mabaharia wakahisi kwamba walikuwa wanakaribia nchi kavu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata usiku wa kumi na nne ulipofika, tulipokuwa tukichukuliwa huku na huko katika bahari ya Adria, kama usiku wa manane baharia wakadhani ya kuwa wanaikaribia nchi kavu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Usiku wa siku ya kumi na nne, tulikuwa tunakokotwa huku na huko katika bahari ya Adria. Karibu na usiku wa manane wanamaji walijihisi kuwa karibu na nchi kavu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Usiku wa kumi na nne ulipofika, nasi tulipotupwa huko na huko katika bahari ya Adiria, usiku wa manene wabaharia wakawaza kwamba: Nchi iko karibu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata usiku wa kumi na nne ulipofika, tulipokuwa tukichukuliwa huko na huko katika bahari ya Adria, kama usiku wa manane baharia wakadhani ya kuwa wanaikaribia nchi kavu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tulieneza majuma mawili tukipelekwa huku na huko na zoruba katika bahari ya Adria. Katikati ya usiku watumishi wa chombo waliwazia kwamba tumekaribia inchi kavu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta usiku wa kumi na nne ulipowadia, tukichukuliwa huko na huko katika bahari ya Adria, usiku wa manane baharia wakadhani ya kuwa wanaikaribia inchi kavu.