Acts 27:28 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo walitafuta kina cha bahari kwa kuteremsha kamba iliyokuwa imefungiwa kitu kizito, wakapata kina cha mita arubaini. Baadaye wakapima tena wakapata mita thelathini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo wakapima kina cha maji na kukuta kilikuwa pima ishirini; baada ya kuendelea mbele kidogo, wakapima tena wakapata kina cha pima kumi na tano.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakatupa bildi wakapata pima ishirini, wakaendelea kidogo wakatupa bildi tena, wakapata pima kumi na tano.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakatupa kamba iliyofungwa kitu kizito kwenye ncha yake. Wakakuta kwamba kina cha maji ni futi mia moja na ishirini. Wakaendelea mbele kidogo na kutupa kamba tena. Kina kilikuwa futi tisini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hivyo walitafuta kina cha bahari kwa kuteremsha kamba iliyokuwa imefungiwa kitu kizito, wakapata kina cha mita arobaini. Baadaye wakapima tena wakapata mita thelathini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo walitafuta kina cha bahari kwa kuteremsha kamba iliyokuwa imefungiwa kitu kizito, wakapata kina cha mita arubaini. Baadaye wakapima tena wakapata mita thelathini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo wakapima kina cha maji na kukuta kilikuwa pima ishirini, baada ya kuendelea mbele kidogo wakapima tena wakapata kina cha pima kumi na tano.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo wakapima kina cha maji na kukuta kilikuwa pima ishirini, baada ya kuendelea mbele kidogo wakapima tena wakapata kina cha pima kumi na tano.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakatupa bildi wakapata pima ishirini, wakaendelea kidogo wakatupa bildi tena, wakapata pima kumi na tano.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo walitafuta kina cha bahari kwa kuteremsha kamba iliyokuwa imefungiwa kitu kizito, wakapata kina cha mita arubaini. Baadaye wakapima tena wakapata mita thelathini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipokishusha kipimo, wakapaona, pana mikono 60. Walipoendelea kidogo, wakakishusha kipimo tena, wakapaona, pana mikono 45.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakatupa bildi wakapata pima ishirini, wakaendelea kidogo wakatupa bildi tena, wakapata pima kumi na tano.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakashusha kipimo ndani ya maji nao wakapata metre makumi ine kwenda chini. Mbali kidogo wakatupa tena kipimo na kupata metre makumi tatu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakatupa bildi wakakuta pima ishirini, wakaendelea kidogo wakatupa bildi tena, wakakuta pima kumi na tano.