Acts 27:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kesho yake tulitia nanga katika bandari ya Sidoni. Yulio alimtendea Paulo vizuri kwa kumruhusu awaone rafiki zake na kupata mahitaji yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kesho yake tukatia nanga Sidoni, naye Juliasi akamfanyia wema Paulo, akamruhusu aende kwa rafiki zake ili wamtimizie mahitaji yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku ya pili tukawasili Sidoni; Yulio akamfadhili sana Paulo akampa ruhusa kwenda kwa rafiki zake, apate kutunzwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku iliyofuata tulifika kwenye mji wa Sidoni. Yulio alikuwa mwema sana kwa Paulo na akampa uhuru wa kwenda kuwatembelea rafiki zake pale, walimpa chochote alichohitaji.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kesho yake tulitia nanga katika bandari ya Sidoni. Yulio alimtendea Paulo vizuri kwa kumruhusu awaone rafiki zake na kupata mahitaji yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kesho yake tulitia nanga katika bandari ya Sidoni. Yulio alimtendea Paulo vizuri kwa kumruhusu awaone rafiki zake na kupata mahitaji yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kesho yake tukatia nanga Sidoni, naye Juliasi akamfanyia wema Paulo, akamruhusu aende kwa rafiki zake ili wampatie mahitaji yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kesho yake tukatia nanga Sidoni, naye Juliasi akamfanyia wema Paulo, akamruhusu aende kwa rafiki zake ili wamtimizie mahitaji yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku iliyofuata tukawasili Sidoni; Yulio akamfadhili sana Paulo akampa ruhusa kwenda kwa rafiki zake, apate kutunzwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kesho yake tulitia nanga katika bandari ya Sidoni. Yulio alimtendea Paulo vizuri kwa kumruhusu awaone rafiki zake na kupata mahitaji yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kesho yake tukafikia Sidoni; Yulio aliyemtunza Paulo kwa upole akampa ruhusa kwenda kwa rafiki zake, apate kugawiwa nao pamba za njiani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku ya pili tukawasili Sidoni; Yulio akamfadhili sana Paulo akampa ruhusa kwenda kwa rafiki zake, apate kutunzwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kesho yake tukatua Sidona. Yulio aliyemutendea Paulo mema, akamupa ruhusa ya kwenda kuonana na warafiki zake, wapate kumupa vitu alivyohitaji.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Siku ya pili tukawasili Sidon; Yulio akamfadhili sana Paolo akampa rukhusa kwenda kwa rafiki zake, kutunzwa nao.