Acts 27:39 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulipokucha, wanamaji hawakuweza kuitambua nchi ile, ila waliona ghuba moja yenye ufuko; wakaamua kutia nanga huko kama ikiwezekana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kulipopambazuka, mabaharia hawakuitambua ile nchi, lakini waliona ghuba yenye ufuko wa mchanga, ambako waliamua kuipweleza meli kama ingewezekana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kulipokucha hawakuitambua ile nchi, ila waliona hori yenye ufuo, wakashauriana kuiegesha merikebu huko, kama ikiwezekana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mchana ulipofika, mabaharia waliiona nchi kavu, lakini hawakupafahamu mahali pale. Waliona ghuba yenye ufukwe na walitaka kuipeleka meli ufukweni ikiwa wangeweza.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kulipokucha, wanamaji hawakuweza kuitambua nchi ile, ila waliona ghuba moja yenye ufuko; wakaamua kutia nanga huko kama ikiwezekana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulipokucha, wanamaji hawakuweza kuitambua nchi ile, ila waliona ghuba moja yenye ufuko; wakaamua kutia nanga huko kama ikiwezekana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kulipopambazuka, mabaharia hawakuitambua ile nchi, lakini waliona ghuba yenye ufuko wa mchanga ambako waliamua kuipweleza meli kama ingewezekana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kulipopambazuka, mabaharia hawakuitambua ile nchi, lakini waliona ghuba yenye ufuko wa mchanga, ambako waliamua kuipweleza meli kama ingewezekana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kulipokucha hawakuitambua ile nchi, ila waliona hori yenye ufuo, wakashauriana kuiegesha merikebu huko, kama ikiwezekana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulipokucha, wanamaji hawakuweza kuitambua nchi ile, ila waliona ghuba moja yenye ufuko; wakaamua kutia nanga huko kama ikiwezekana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kulipokucha, hawakuitambua nchi. Lakini walipoona kituo penye ufuko, wakataka kukiingiza chombo huko, ikiwezekana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kulipokucha hawakuitambua ile nchi, ila waliona hori yenye ufuo, wakashauriana kuiegesha merikebu huko, kama ikiwezekana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulipokucha wabaharia hawakutambua inchi ile lakini wakaona nafasi bahari inapoingia ndani ya inchi kavu na kwenye kivuko. Basi wakakusudia kwenda kukwamisha chombo kule, kama ikiwezekana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kulipokucha hawakuitambua ile inchi, illa waliona hori yenye ufuko, wakashauriana kuiegesha merikebu huko, kama ikiwezekana.