Acts 27:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutoka huko tuliendelea na safari, lakini kwa kuwa upepo ulikuwa unavuma kwa kasi kutujia kwa mbele, tulipitia upande wa kisiwa cha Kupro ambapo upepo haukuwa mwingi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutoka huko tukaingia baharini tena na tukapita upande wa chini wa kisiwa cha Kipro kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kutoka huko tukatweka, tukasafiri chini ya Kipro ili kuukinga upepo, kwa maana pepo zilikuwa za mbisho.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tuliondoka katika mji ule na tukatweka tanga tukasafiri karibu na kisiwa cha Kipro kwa sababu upepo ulikuwa unavuma kinyume nasi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kutoka huko tuliendelea na safari, lakini kwa kuwa upepo ulikuwa unavuma kwa kasi kutujia kwa mbele, tulipitia upande wa kisiwa cha Kupro ambapo upepo haukuwa mwingi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutoka huko tuliendelea na safari, lakini kwa kuwa upepo ulikuwa unavuma kwa kasi kutujia kwa mbele, tulipitia upande wa kisiwa cha Kupro ambapo upepo haukuwa mwingi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka huko tukaingia baharini tena na tukapita upande wa chini wa kisiwa cha Kipro kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka huko tukaingia baharini tena na tukapita upande wa chini wa kisiwa cha Kipro kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kutoka huko tukiwa baharini, tukasafiri chini ya Kipro ili kujikinga upepo, kwa maana upepo ulikuwa unatukabili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kutoka huko tuliendelea na safari, lakini kwa kuwa upepo ulikuwa unavuma kwa kasi kutujia kwa mbele, tulipitia upande wa kisiwa cha Kupro ambapo upepo haukuwa mwingi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tulipotweka huko tukakielekeza chombo kwenda kandokando ya Kipuro, kwa sababu pepo zilitujia mbele.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kutoka huko tukatweka, tukasafiri chini ya Kipro ili kuukinga upepo, kwa maana pepo zilikuwa za mbisho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutoka kule, tukapita pembenipembeni ya kisanga cha Kipuro kwa kuepuka upepo uliokuwa ukivuma tokea mbele yetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kutoka huko tukatweka, tukasafiri chini ya Kupro illi kuukinga upepo, kwa maana pepo zilikuwa za mbisho,