Acts 27:40 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo walikata nanga na kuziacha baharini, na wakati huohuo wakazifungua kamba zilizokuwa zimeufunga usukani, kisha wakatweka tanga moja mbele kushika upepo, wakaelekea ufukoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo wakatupa nanga zote na kuziacha baharini, na wakati huo huo wakalegeza kamba zilizokuwa zikishikilia usukani wa meli. Kisha wakatweka tanga la mbele lishike upepo na kuisukuma meli kuelekea pwani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakazitupilia mbali zile nanga, na kuziacha baharini, pamoja na kuzilegeza kamba za sukani, wakalitweka tanga dogo ili liushike upepo, wakauendea ule ufuo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo walikata kamba kwenye nanga na kuziacha nanga ndani ya bahari. Wakati huo huo walifungua kamba zilizokuwa zinaushikilia usukani. Kisha wakanyanyua tanga la mbele na kutweka tanga kuelekea ufukweni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hivyo walikata nanga na kuziacha baharini, na wakati huohuo wakazifungua kamba zilizokuwa zimeufunga usukani, kisha wakatweka tanga moja mbele kushika upepo, wakaelekea ufukoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo walikata nanga na kuziacha baharini, na wakati huohuo wakazifungua kamba zilizokuwa zimeufunga usukani, kisha wakatweka tanga moja mbele kushika upepo, wakaelekea ufukoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo wakatupa nanga zote na kuziacha baharini, wakati huo huo wakalegeza kamba zilizokuwa zikishikilia usukani wa meli, kisha wakatweka tanga la mbele lishike upepo na kuisukuma meli kuelekea pwani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo wakatupa nanga zote na kuziacha baharini, na wakati huo huo wakalegeza kamba zilizokuwa zikishikilia usukani wa meli. Kisha wakatweka tanga la mbele lishike upepo na kuisukuma meli kuelekea pwani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakazitupilia mbali zile nanga, na kuziacha baharini, pamoja na kuzilegeza kamba za sukani, wakalitweka tanga dogo ili liushike upepo, wakauendea ule ufuo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo walikata nanga na kuziacha baharini, na wakati huohuo wakazifungua kamba zilizokuwa zimeufunga usukani, kisha wakatweka tanga moja mbele kushika upepo, wakaelekea ufukoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakazikata kamba za nanga, wakaziacha baharini; hapohapo wakazilegeza nazo kamba zilizofunga sukani, wakatweka tanga dogo na kulielekezea upepo, wakaufuata ufuko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakazitupilia mbali zile nanga, na kuziacha baharini, pamoja na kuzilegeza kamba za sukani, wakalitweka tanga dogo ili liushike upepo, wakauendea ule ufuo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakafungua nanga na kuziachilia zizame ndani ya bahari. Vilevile waliregeza kamba za makasia ya kuongoza chombo. Kisha wakafunga tanga ndogo mbele ya chombo kusudi kipelekwe na upepo, nao wakaelekea kwenye kile kivuko.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakazitupilia mbali zile nanga, wakaziacha baharini, wakazilegeza kamba za sukani, wakalitweka tanga dogo illi liushike upepo, wakauendea ule ufuko.