Acts 27:41 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini walifika mahali ambapo mikondo miwili ya bahari hukutana, na meli ikakwama. Sehemu ya mbele ilikuwa imezama mchangani bila kutikisika. Sehemu ya nyuma ya meli ilianza kuvunjika vipandevipande kwa mapigo ya nguvu ya mawimbi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wakafika mahali bahari mbili zinakutana, wakaipweleza meli ufuoni; omo ikakwama sana, ikawa haiwezi kuondolewa; lakini sehemu ya shetri ikavunjika vipande vipande kutokana na kupigwa kwa mawimbi yenye nguvu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini wakafikia mahali palipokutana bahari mbili, wakaiegesha merikebu, omo ikakwama ikakaa isitikiswe, bali tezi ilikuwa imefumuliwa kwa nguvu za mawimbi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini meli uligonga mwamba wa michanga. Sehemu ya mbele ya meli ilikwama pale na haikuweza kutoka. Kisha mawimbi makubwa yakaanza kuvunja sehemu ya nyuma ya meli vipande vipande.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini walifika mahali ambapo mikondo miwili ya bahari hukutana, na meli ikakwama. Sehemu ya mbele ilikuwa imezama mchangani bila kutikisika. Sehemu ya nyuma ya meli ilianza kuvunjika vipandevipande kwa mapigo ya nguvu ya mawimbi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini walifika mahali ambapo mikondo miwili ya bahari hukutana, na meli ikakwama. Sehemu ya mbele ilikuwa imezama mchangani bila kutikisika. Sehemu ya nyuma ya meli ilianza kuvunjika vipandevipande kwa mapigo ya nguvu ya mawimbi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wakafika mahali ambapo bahari mbili zinakutana, wakaipweleza meli ufuoni, omo ikakwama sana, ikawa haiwezi kuondolewa, lakini sehemu ya shetri ikavunjika vipande vipande kwa kule kupiga kwa mawimbi yenye nguvu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wakafika mahali ambapo bahari mbili zinakutana, wakaipweleza meli ufuoni, omo ikakwama sana, ikawa haiwezi kuondolewa, lakini sehemu ya shetri ikavunjika vipande vipande kwa kule kupiga kwa mawimbi yenye nguvu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini wakafikia mahali palipokutana bahari mbili, wakaiegesha merikebu, humo ikakwama ikakaa isitikiswe, bali tezi ilikuwa imefumuliwa kwa nguvu za mawimbi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini walifika mahali ambapo mikondo miwili ya bahari hukutana, na meli ikakwama. Sehemu ya mbele ilikuwa imezama mchangani bila kutikisika. Sehemu ya nyuma ya meli ilianza kuvunjika vipandevipande kwa mapigo ya nguvu ya mawimbi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini tulitupwa funguni, chombo kikakwama mbele, kikachimba mchangani, kikashikwa kabisa, kisitukutike hata kidogo, lakini nyuma kikavunjwa kwa nguvu ya mawimbi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wakafikia mahali palipokutana bahari mbili, wakaiegesha merikebu, omo ikakwama ikakaa isitikiswe, bali tezi ilikuwa imefumuliwa kwa nguvu za mawimbi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wakakwama kwenye lundo ya muchanga na chombo kikakwama pale. Sehemu ya mbele ya chombo ikazama kabisa pasipo kutikisika, lakini sehemu ya nyuma ikavunjikavunjika kwa kupigwa na zoruba kwa nguvu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini wakafikia mahali palipokutana bahari mbili, wakaiegesha merikebu, omo ikakwama ikakaa isitikiswe, bali shetri ilikuwa imefumuliwa kwa nguvu za mawimbi.