Acts 27:43 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kwa vile yule ofisajeshi alitaka kumwokoa Paulo, aliwazuia wasifanye hivyo. Aliamuru wale waliojua kuogelea waruke kutoka melini na kuogelea hadi pwani,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini yule jemadari alitaka kuokoa maisha ya Paulo, basi akawazuia askari wasitekeleze mpango wao. Akaamuru wale wanaoweza kuogelea wajitupe baharini kwanza, waogelee hadi nchi kavu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali akida, akitaka kumponya Paulo, akawazuia, wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea wajitupe kwanza baharini, wafike nchi kavu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Yulio, ofisa wa jeshi alitaka Paulo asiuawe. Hivyo hakuwaruhusu askari kuwaua wafunga. Aliwaambia watu wanaoweza kuogelea, waruke majini kwenda nchi kavu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini kwa vile yule ofisajeshi alitaka kumwokoa Paulo, aliwazuia wasifanye hivyo. Aliamuru wale waliojua kuogelea waruke kutoka melini na kuogelea hadi pwani,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kwa vile yule ofisajeshi alitaka kumwokoa Paulo, aliwazuia wasifanye hivyo. Aliamuru wale waliojua kuogelea waruke kutoka melini na kuogelea hadi pwani,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini yule jemadari akitaka kuokoa maisha ya Paulo, akawazuia maaskari wasitekeleze mpango wao. Akaamuru wale wanaoweza kuogelea wajitupe baharini kwanza, waogelee mpaka nchi kavu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini yule jemadari alitaka kuokoa maisha ya Paulo, basi akawazuia askari wasitekeleze mpango wao. Akaamuru wale wanaoweza kuogelea wajitupe baharini kwanza, waogelee mpaka nchi kavu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali ofisa, akitaka kumponya Paulo, akawazuia, wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea wajitupe kwanza baharini, wafike katika nchi kavu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kwa vile yule ofisajeshi alitaka kumwokoa Paulo, aliwazuia wasifanye hivyo. Aliamuru wale waliojua kuogelea waruke kutoka melini na kuogelea hadi pwani,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
bwana askari alitaka kumwokoa Paulo, akawazuia, wasivifanye, walivyovitaka; kisha akawaagiza wanaojua kuogelea, wajitupe wa kwanza baharini, wafike pwani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali akida, akitaka kumponya Paulo, akawazuia, wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea wajitupe kwanza baharini, wafike nchi kavu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kwa kuwa mukubwa wa jeshi alitaka kumuponyesha Paulo, yeye akawazuiza wasitimize kusudi lao. Akaamuru wale waliojua kuogelea wajitupe wa kwanza ndani ya maji na kuvuka mpaka inchi kavu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bali akida, akitaka kumponya Paolo, akawazuia, wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea wajitupe baharini, wafike inchi kavu;