Acts 27:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Muda mrefu ulikuwa umepita, na hata siku ya kufunga ilikuwa imekwisha pita. Sasa ilikuwa hatari sana kusafiri kwa meli. Basi, Paulo aliwapa onyo:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Muda mwingi ulikuwa umepotea, na kusafiri baharini kulikuwa hatari, kwa sababu wakati huu ulikuwa baada ya Siku ya Kufunga. Hivyo Paulo akawaonya akasema,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wakati mwingi ulipokwisha kupita, na safari ikiwa ina hatari sasa, kwa sababu siku za kufunga zilikuwa zimekwisha kupita, Paulo akawaonya,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tulikuwa tumepoteza muda mwingi, na ilikuwa hatari kutweka tanga, kwa sababu tayari ilikuwa baada ya siku ya Kiyahudi ya kufunga. Hivyo Paulo aliwaonya akasema,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Muda mrefu ulikuwa umepita, na hata siku ya kufunga ilikuwa imekwisha pita. Sasa ilikuwa hatari sana kusafiri kwa meli. Basi, Paulo aliwapa onyo:
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Muda mrefu ulikuwa umepita, na hata siku ya kufunga ilikuwa imekwisha pita. Sasa ilikuwa hatari sana kusafiri kwa meli. Basi, Paulo aliwapa onyo:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Muda mwingi ulikuwa umepotea na kusafiri baharini kulikuwa hatari kwa sababu wakati huu ulikuwa baada ya siku za kufunga. Hivyo Paulo akawaonya akasema,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Muda mwingi ulikuwa umepotea na kusafiri baharini kulikuwa hatari kwa sababu wakati huu ulikuwa baada ya siku za kufunga. Hivyo Paulo akawaonya akasema,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wakati mwingi ulipokwisha kupita, na safari ikiwa ina hatari sasa, kwa sababu siku za kufunga zilikuwa zimekwisha kupita, Paulo akawaonya,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Muda mrefu ulikuwa umepita, na hata siku ya kufunga ilikuwa imekwisha pita. Sasa ilikuwa hatari sana kusafiri kwa meli. Basi, Paulo aliwapa onyo:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo siku zilizopita zikawa nyingi, tena kwenda baharini siku zile kukaponza watu wana, kwa sababu hata siku za kufunga zilikuwa zimepita. Paulo akawaonya
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wakati mwingi ulipokwisha kupita, na safari ikiwa ina hatari sasa, kwa sababu siku za kufunga zilikuwa zimekwisha kupita, Paulo akawaonya,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha kupitisha siku nyingi, tukafikia katika nyakati za hatari za safari ya bahari, kwa maana siku ya kufunga kula ilikuwa imekwisha kupita. Halafu Paulo akatupatia shauri hili:
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na wakati mwingi ulipokwisha kupita, na safari ikiwa ina khatari sasa kwa sababu siku za kufunga zilikuwa zimekwisha kupita, Paolo akawaonya, akawaambia,