Acts 28:11 — Compare Translations

13 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya miezi mitatu tulianza tena safari yetu kwa meli moja ya Aleksandria iitwayo “Miungu Pacha”. Meli hiyo ilikuwa imetia nanga kisiwani wakati wote wa baridi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Miezi mitatu baadaye tukaanza safari kwa meli iliyokuwa imetia nanga kwenye kisiwa hicho kwa ajili ya majira ya baridi. Hii ilikuwa meli ya Iskanderia yenye alama ya miungu pacha waitwao Kasta na Poluksi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Iskanderia iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Ndugu Pacha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya miezi mitatu tulianza tena safari yetu kwa meli moja ya Aleksandria iitwayo “Miungu Pacha”. Meli hiyo ilikuwa imetia nanga kisiwani wakati wote wa baridi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya miezi mitatu tulianza tena safari yetu kwa meli moja ya Aleksandria iitwayo “Miungu Pacha”. Meli hiyo ilikuwa imetia nanga kisiwani wakati wote wa baridi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Miezi mitatu baadaye tukaanza safari kwa meli iliyokuwa imetia nanga kwenye kisiwa hicho kwa ajili ya majira ya baridi. Hii ilikuwa meli ya Aleksandria yenye alama ya miungu pacha waitwao Kasta na Poluksi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Miezi mitatu baadaye tukaanza safari kwa meli iliyokuwa imetia nanga kwenye kisiwa hicho kwa ajili ya majira ya baridi. Hii ilikuwa meli ya Iskanderia yenye alama ya miungu pacha waitwao Kasta na Poluksi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Aleksandria iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Ndugu Pacha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya miezi mitatu tulianza tena safari yetu kwa meli moja ya Aleksandria iitwayo “Miungu Pacha”. Meli hiyo ilikuwa imetia nanga kisiwani wakati wote wa baridi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Miezi mitatu ilipopita, tukaondoka tukijipakia chomboni kilichotoka Alekisandria; kilikuwa kimezimaliza siku za kipupwe pale kisiwani; kilikuwa chenye chapa cha mapacha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Iskanderia iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Ndugu Pacha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulipopita miezi mitatu, tukasafiri katika chombo kimoja kilichobaki katika kisanga kile kwa kungojea wakati wa baridi kali upite kwanza. Chombo kile kilikuwa chenye kutoka Alesanduria. Na juu yake kulikuwa michoro ya sanamu za mapacha ya miungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Iskanderia iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Dioskuri.