Acts 28:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Toka huko tulingoa nanga, tukazunguka na kufika Regio. Baada ya siku moja, upepo ulianza kuvuma kutoka kusini, na baada ya siku mbili tulifika bandari ya Potioli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha tukang’oa nanga, tukafika Regio. Siku iliyofuata, upepo mkali wa kusi ukavuma, na siku ya pili yake tukafika Puteoli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kutoka huko tukazunguka tukafikia Regio; baada ya siku moja upepo wa kusi ukavuma, na siku ya pili tukawasili Puteoli.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tulifika katika mji wa Regio. Siku iliyofuata upepo ulianza kuvuma kutokea Kusini-Magharibi, hivyo tuliweza kuondoka. Baada ya siku moja tukafika katika mji wa Puteoli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Toka huko tuling'oa nanga, tukazunguka na kufika Regio. Baada ya siku moja, upepo ulianza kuvuma kutoka kusini, na baada ya siku mbili tulifika bandari ya Potioli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Toka huko tuling'oa nanga, tukazunguka na kufika Regio. Baada ya siku moja, upepo ulianza kuvuma kutoka kusini, na baada ya siku mbili tulifika bandari ya Potioli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha tukang'oa nanga tukafika Regio siku iliyofuata, upepo mkali wa kusi ukavuma, na siku ya pili yake tukafika Puteoli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha tukang’oa nanga, tukafika Regio. Siku iliyofuata, upepo mkali wa kusi ukavuma, na siku ya pili yake tukafika Puteoli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kutoka huko tukazunguka tukafikia Regio; baada ya siku moja upepo wa kusi ukavuma, na siku ya pili tukawasili Puteoli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Toka huko tulingoa nanga, tukazunguka na kufika Regio. Baada ya siku moja, upepo ulianza kuvuma kutoka kusini, na baada ya siku mbili tulifika bandari ya Potioli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kutoka huko tukazunguka, tukafika Regio. Tulipongoja siku moja, kukavuma upepo wa kusini, tukafika Puteoli kwa mwendo wa siku mbili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kutoka huko tukazunguka tukafikia Regio; baada ya siku moja upepo wa kusi ukavuma, na siku ya pili tukawasili Puteoli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutoka kule tukazunguka pembenipembeni ya bahari hata tukafika katika muji Regio. Kesho yake upepo usiokuwa mukali ukaanza kuvuma tokea kusini, na kwa mwendo wa siku mbili tukafika katika muji Puteoli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kutoka huko tukazunguka tukafikia Regio: baada ya siku moja upepo wa kusi ukavuma, na siku ya pili tukawasili Puteoli.