Acts 28:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Wayahudi wengine walipinga jambo hilo, nami nikalazimika kukata rufani kwa Kaisari, ingawa sikuwa na chochote cha kuwashtaki wananchi wenzangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Wayahudi walipopinga uamuzi huo, nililazimika kukata rufaa kwa Kaisari, ingawa sikuwa na lalamiko lolote juu ya taifa langu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Wayahudi walipotoa hoja juu ya shauri hili nalishurutishwa kutaka rufani kwa Kaisari. Si kwamba nalikuwa na neno la kuwashitaki watu wa taifa langu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Wayahudi kule hawakutaka hilo. Hivyo ilinibidi niombe kuja Rumi kuweka mashitaka yangu mbele ya Kaisari. Kwa kufanya hivi haimaanishi kuwa ninawashutumu watu wangu kwa kufanya chochote kibaya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Wayahudi wengine walipinga jambo hilo, nami nikalazimika kukata rufani kwa Kaisari, ingawa sikuwa na chochote cha kuwashtaki wananchi wenzangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Wayahudi wengine walipinga jambo hilo, nami nikalazimika kukata rufani kwa Kaisari, ingawa sikuwa na chochote cha kuwashtaki wananchi wenzangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Wayahudi walipopinga uamuzi huo, nililazimika kukata rufaa kwa Kaisari, ingawa sikuwa na lalamiko lo lote juu ya taifa langu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Wayahudi walipopinga uamuzi huo, nililazimika kukata rufaa kwa Kaisari, ingawa sikuwa na lalamiko lolote juu ya taifa langu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Wayahudi walipotoa hoja juu ya shauri hili nilishurutishwa kutaka rufani kwa Kaisari. Si kwamba nilikuwa na neno la kuwashitaki watu wa taifa langu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Wayahudi wengine walipinga jambo hilo, nami nikalazimika kukata rufani kwa Kaisari, ingawa sikuwa na chochote cha kuwashtaki wananchi wenzangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Wayuda walipobisha, nikashurutishwa kutaka kuhukumiwa na Kaisari, lakini hapo siko kwamba: Niwasute walio wa taifa langu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Wayahudi walipotoa hoja juu ya shauri hili nalishurutishwa kutaka rufani kwa Kaisari. Si kwamba nalikuwa na neno la kuwashitaki watu wa taifa langu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini nilipoona kwamba Wayuda wanakataa shauri lile, ilinilazimisha kuomba nisambishwe na Mufalme wa Roma. Na katika haya yote sikukuwa na mashitaki yoyote juu ya taifa langu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini Wayahudi walipotoa hoja juu ya shauri hili nalishurutishwa kutaka rufaani kwa Kaisari. Si kwamba nalikuwa na neno la kuwashitaki watu wa taifa langu.