Acts 28:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wao wakamwambia, “Sisi hatujapokea barua yoyote kutoka Yudea, wala hakuna ndugu yeyote aliyefika hapa na kutoa habari rasmi au kusema chochote kibaya juu yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamjibu, “Hatujapokea barua zozote kutoka Yudea zinazokuhusu, wala hapana ndugu yeyote aliyekuja hapa ambaye ametoa taarifa au kuzungumza jambo lolote baya juu yako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wale wakamwambia, Sisi hatukupata nyaraka zenye habari zako kutoka Uyahudi, wala hapana ndugu hata mmoja aliyefika hapa na kutupasha habari, au kunena neno baya juu yako.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wayahudi walimjibu Paulo, “Hakuna barua tuliyoipokea kutoka Uyahudi kuhusu wewe. Hakuna ndugu yetu yeyote Myahudi aliyesafiri kutoka huko aliyeleta habari zako au kutwambia chochote kibaya juu yako.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wao wakamwambia, “Sisi hatujapokea barua yoyote kutoka Yudea, wala hakuna ndugu yeyote aliyefika hapa na kutoa habari rasmi au kusema chochote kibaya juu yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wao wakamwambia, “Sisi hatujapokea barua yoyote kutoka Yudea, wala hakuna ndugu yeyote aliyefika hapa na kutoa habari rasmi au kusema chochote kibaya juu yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamjibu, “Hatujapokea barua zo zote kutoka Uyahudi zinazokuhusu, wala hapana ndugu ye yote aliyekuja hapa ambaye ametoa taarifa au kuzungumza jambo lo lote baya juu yako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamjibu, “Hatujapokea barua zozote kutoka Uyahudi zinazokuhusu, wala hapana ndugu yeyote aliyekuja hapa ambaye ametoa taarifa au kuzungumza jambo lolote baya juu yako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wale wakamwambia, Sisi hatukupata nyaraka zenye habari zako kutoka Yudea, wala hapana ndugu hata mmoja aliyefika hapa na kutupasha habari, au kunena neno baya juu yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wao wakamwambia, “Sisi hatujapokea barua yoyote kutoka Yudea, wala hakuna ndugu yeyote aliyefika hapa na kutoa habari rasmi au kusema chochote kibaya juu yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wakamwambia: Sisi kwa ajili yako hatukupata barua toka Yudea, wala hakuna ndugu aliyetujia na kutusimulia mambo yako, wala kusema kibaya, ulichokifanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wale wakamwambia, Sisi hatukupata nyaraka zenye habari zako kutoka Uyahudi, wala hapana ndugu hata mmoja aliyefika hapa na kutupasha habari, au kunena neno baya juu yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamwambia: “Sisi hatukupokea barua juu yako toka Yudea, wala ndugu Muyuda aliyefika huku kwa kutupasha habari, wala kusema ubaya juu yako.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wale wakamwambia, Sisi hatukupata nyaraka zenye khabari zako kutoka Yahudi, wala hapana ndugu hatta mmoja aliyefika hapa na kutupasha khabari, au kunena neno baya juu yako.