Acts 28:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kukawa na mtengano wa fikira kati yao. Walipokuwa wanakwenda zao, Paulo alisema jambo hili: “Kweli ni sawa yale Roho Mtakatifu aliyowaarifu wazee wenu kwa njia ya nabii Isaya
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo hawakukubaliana, nao walipokuwa wanaondoka, Paulo akatoa kauli moja zaidi: “Roho wa Mungu alinena kweli na baba zenu aliposema mambo yale yaliyomhusu Bwana Isa kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na walipokuwa hawapatani wao kwa wao, wakaenda zao, Paulo alipokwisha kusema neno hili moja, ya kwamba, Roho Mtakatifu alinena vema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walibishana wao wenyewe na wakaanza kuondoka. Lakini aliwaambia kitu kimoja zaidi: “Roho Mtakatifu aliwaambia ukweli baba zenu kupitia nabii Isaya, aliposema,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, kukawa na mtengano wa fikira kati yao. Walipokuwa wanakwenda zao, Paulo alisema jambo hili, “Kweli ni sawa yale aliyoyanena Roho Mtakatifu kwa wazee wenu kwa njia ya nabii Isaya
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kukawa na mtengano wa fikira kati yao. Walipokuwa wanakwenda zao, Paulo alisema jambo hili: “Kweli ni sawa yale Roho Mtakatifu aliyowaarifu wazee wenu kwa njia ya nabii Isaya
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo hawakukubaliana, nao walipokuwa wanaondoka, Paulo akatoa kauli moja zaidi: “Roho Mtakatifu alinena kweli na baba zenu aliposema mambo yale yaliyomhusu Bwana Yesu kwa kinywa cha Isaya kwamba:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo hawakukubaliana, nao walipokuwa wanaondoka, Paulo akatoa kauli moja zaidi: “Roho wa Mwenyezi Mungu alinena kweli na baba zenu aliposema mambo yale yaliyomhusu Bwana Isa kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na walipokuwa hawapatani wao kwa wao, wakaenda zao, Paulo alipokwisha kusema neno hili moja, ya kwamba, Roho Mtakatifu alinena vema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kukawa na mtengano wa fikira kati yao. Walipokuwa wanakwenda zao, Paulo alisema jambo hili: “Kweli ni sawa yale Roho Mtakatifu aliyowaarifu wazee wenu kwa njia ya nabii Isaya
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo wakashindwa kupatana wao kwa wao, wakajiendea zao. Ndipo, Paulo aliposema neno kwa kinywa cha mfumbuaji Yesaya:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na walipokuwa hawapatani wao kwa wao, wakaenda zao, Paulo alipokwisha kusema neno hili moja, ya kwamba, Roho Mtakatifu alinena vema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao walipokuwa wakiondoka bila kupatana, Paulo akaongeza kuwaambia maneno haya tu: “Roho Mutakatifu alikuwa na sheria ya kusema hivi kwa babu zenu kwa njia ya nabii Isaya:
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na walipokuwa hawapatani wao kwawao, wakaenda zao, Paolo alipokwisha kusema neno hili moja ya kama, Roho Mtakatifu alinena vema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya,