Acts 28:27 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana akili za watu hawa zimepumbaa, wameziba masikio yao, wamefumba macho yao. La sivyo, wangeona kwa macho yao, wangesikia kwa masikio yao. Wangeelewa kwa akili zao, na kunigeukia, asema Bwana, nami ningewaponya.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu; hawasikii kwa masikio yao, na wamefumba macho yao. Wasije wakaona kwa macho yao, na wakasikiliza kwa masikio yao, wakaelewa kwa mioyo yao, na kugeuka nami nikawaponya.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana mioyo ya watu hawa imepumbaa, Na masikio yao ni mazito ya kusikia, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Na kusikia kwa masikio yao, Na kufahamu kwa mioyo yao, Na kubadili nia zao, nikawaponya.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu hawa hawawezi kuelewa. Masikio yao yamezibwa. Na macho yao yamefumbwa. Hivyo hawawezi kuona kwa macho yao, au kusikia kwa masikio yao; au kuelewa kwa akili zao; au kuelewa kwa akili zao. Ikiwa wangeelewa, wangeweza kunirudia, na ningewaponya.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana akili za watu hawa zimepumbaa, wameziba masikio yao, wamefumba macho yao. La sivyo, wangeona kwa macho yao, wangesikia kwa masikio yao. Wangeelewa kwa akili zao, na kunigeukia, asema Bwana, nami ningewaponya.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana akili za watu hawa zimepumbaa, wameziba masikio yao, wamefumba macho yao. La sivyo, wangeona kwa macho yao, wangesikia kwa masikio yao. Wangeelewa kwa akili zao, na kunigeukia, asema Bwana, nami ningewaponya.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu, na masikio yao ni mazito kusikia, nao wamefumba macho yao. Wasije wakaona kwa macho yao, na kusikiliza kwa masikio yao, wakaelewa kwa mioyo yao na kugeuka, nami nikawaponya.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu; hawasikii kwa masikio yao, na wamefumba macho yao. Wasije wakaona kwa macho yao, na wakasikiliza kwa masikio yao, wakaelewa kwa mioyo yao, na kugeuka nami nikawaponya.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana mioyo ya watu hawa imepumbaa, Na masikio yao ni mazito ya kusikia, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Na kusikia kwa masikio yao, Na kufahamu kwa mioyo yao, Na kubadili nia zao, nikawaponya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana akili za watu hawa zimepumbaa, wameziba masikio yao, wamefumba macho yao. La sivyo, wangeona kwa macho yao, wangesikia kwa masikio yao. Wangeelewa kwa akili zao, na kunigeukia, asema Bwana, nami ningewaponya.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mioyo yao walio ukoo huu imeshupazwa, wasisikie kwa masikio yao yaliyo mazito, nayo macho yao wameyasinziza, wasije wakaona kwa macho yao, au wakasikia kwa masikio yao, au wakajua maana kwa mioyo yao, wakanigeukia, nikawaponya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana mioyo ya watu hawa imepumbaa, Na masikio yao ni mazito ya kusikia, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Na kusikia kwa masikio yao, Na kufahamu kwa mioyo yao, Na kubadili nia zao, nikawaponya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana mioyo ya watu hawa imegeuka kuwa migumu, wameziba masikio yao na wamefunga macho yao. Isingekuwa hivi, wangeona na macho yao, wangesikia na masikio yao, wangefahamu na mioyo yao, na wangegeukia kwangu na ningewaponyesha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana mioyo ya watu hawa imepumbaa, Na masikio yao ni wazito wa kusikia, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Na kusikia kwa masikio yao, Na kufahamu kwa mioyo yao, Na kuhadili nia zao Nikawaponya.