Acts 28:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Paulo aliokota mzigo mdogo wa kuni akawa anazitia motoni. Hapo, kwa sababu ya lile joto la moto, nyoka akatoka katika kuni akamnasa Paulo mkononi na kujishikilia hapo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Paulo alikusanya mzigo wa kuni, na alipokuwa anaweka kuni kwenye moto, nyoka mwenye sumu akatoka humo kwa ajili ya joto na kujisokotea mkononi mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Paulo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni, na kuuweka motoni, nyoka akatoka kwa ajili ya ule moto akamzonga-zonga mkononi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Paulo alikusanya kuni nyingi kwa ajili ya moto. Alipokuwa akiweka kuni kwenye moto, nyoka mwenye sumu kali akajitokeza kwa sababu ya joto na kumuuma kwenye mkono.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Paulo aliokota mzigo mdogo wa kuni akawa anazitia motoni. Hapo, kwa sababu ya lile joto la moto, nyoka akatoka katika kuni akamnasa Paulo mkononi na kujishikilia hapo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Paulo aliokota mzigo mdogo wa kuni akawa anazitia motoni. Hapo, kwa sababu ya lile joto la moto, nyoka akatoka katika kuni akamnasa Paulo mkononi na kujishikilia hapo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Paulo alikuwa amekusanya mzigo wa kuni na alipokuwa anaweka kwenye moto kwa ajili ya joto, nyoka mwenye sumu akatoka humo na kujisokotea mkononi mwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Paulo alikuwa amekusanya mzigo wa kuni na alipokuwa anaweka kwenye moto kwa ajili ya joto, nyoka mwenye sumu akatoka humo na kujisokotea mkononi mwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Paulo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni, na kuuweka motoni, nyoka akatoka kwa ajili ya ule moto akamzongazonga mkononi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Paulo aliokota mzigo mdogo wa kuni akawa anazitia motoni. Hapo, kwa sababu ya lile joto la moto, nyoka akatoka katika kuni akamnasa Paulo mkononi na kujishikilia hapo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Paulo alipodondoa mzigo wa vijiti kuvitia motoni, mkatoka humo nyoka kwa ajili ya moto, akamzingazinga mkono.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Paulo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni, na kuuweka motoni, nyoka akatoka kwa ajili ya ule moto akamzonga-zonga mkononi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Paulo akatwaa lundo ya kuni, na alipokuwa akiiweka ndani ya moto, nyoka akatoka katikati ya ile lundo kwa sababu ya kivukuto na kujizingia kwa mukono wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Paolo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni, na kuuweka juu ya moto, nyoka akatoka kwa ajili ya ule moto, akamzingisha katika mkono wake.