Acts 28:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wenyeji wa pale walipokiona kile kiumbe kinaninginia kwenye mkono wake waliambiana, “Bila shaka mtu huyu amekwisha ua mtu, na ingawa ameokoka kuangamia baharini, ‘Haki’ haitamwacha aendelee kuishi!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale wenyeji wa kile kisiwa walipomwona yule nyoka akining’inia mkononi mwa Paulo, wakaambiana, “Huyu mtu lazima awe ni muuaji, ingawa ameokoka kutoka baharini, haki haijamwacha aishi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wenyeji walipomwona yule nyoka akilewa-lewa mkononi, wakaambiana, Hakosi mtu huyu ni mwuaji; ambaye ijapokuwa ameokoka katika bahari haki haimwachi kuishi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wenyeji wa kisiwa kile walipomwona nyoka ananing'inia kwenye mkono wa Paulo, walisema, “Mtu huyu lazima ni mwuaji! Hakufa baharini, lakini Haki hataki aishi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wenyeji wa pale walipokiona kile kiumbe kinaning'inia kwenye mkono wake waliambiana, “Bila shaka mtu huyu amekwisha ua mtu, na ingawa ameokoka kuangamia baharini, Haki haitamwacha aendelee kuishi!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wenyeji wa pale walipokiona kile kiumbe kinaning'inia kwenye mkono wake waliambiana, “Bila shaka mtu huyu amekwisha ua mtu, na ingawa ameokoka kuangamia baharini, ‘Haki’ haitamwacha aendelee kuishi!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale wenyeji wa kile kisiwa walipomwona yule nyoka akining'inia mkononi mwa Paulo, wakaambiana, “Huyu mtu lazima awe ni mwuaji, ingawa ameokoka kutoka baharini, haki haijamwacha aishi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale wenyeji wa kile kisiwa walipomwona yule nyoka akining’inia mkononi mwa Paulo, wakaambiana, “Huyu mtu lazima awe ni muuaji, ingawa ameokoka kutoka baharini, haki haijamwacha aishi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wenyeji walipomwona yule nyoka akilewalewa mkononi, wakaambiana, Hakosi mtu huyu ni mwuaji; ambaye ijapokuwa ameokoka katika bahari haki haimwachi kuishi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wenyeji wa pale walipokiona kile kiumbe kinaninginia kwenye mkono wake waliambiana, “Bila shaka mtu huyu amekwisha ua mtu, na ingawa ameokoka kuangamia baharini, ‘Haki’ haitamwacha aendelee kuishi!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wenyeji walipomwona yule mdudu, alivyomng'ang'ania mkononi pake, wakasemezana wao kwa wao: Mtu huyu hakosi kuwa mwuaji, kwani ingawa ameokoka baharini, tena lipizi halimwachi, awepo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wenyeji walipomwona yule nyoka akilewa-lewa mkononi, wakaambiana, Hakosi mtu huyu ni mwuaji; ambaye ijapokuwa ameokoka katika bahari haki haimwachi kuishi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale wenyeji wa kule walipoona nyoka yule anajizingia kwa mukono wake wakasemezana: “Hakika mutu huyu ni mwuaji, kwa maana ijapokuwa alipona katika hatari ya bahari, kufuatana na azabu ya haki ya Mungu, kufa kwake kunatimia.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Washenzi walipomwona yule nyoka akimwangikia mkono, wakaambiana, Hakosi mtu huyu ni muuaji; na ijapokuwa ameokoka katika bahari, haki haimwachi kuishi.