Acts 28:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale watu walikuwa wakitazamia kwamba angevimba au angeanguka chini na kufa ghafla. Baada ya kungojea kwa muda mrefu bila kuona kwamba Paulo amepatwa na jambo lolote lisilo la kawaida, walibadilisha fikira zao juu yake, wakasema kuwa yeye ni mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu walikuwa wanangoja avimbe au aanguke ghafula na kufa. Lakini baada ya kungoja kwa muda mrefu na kuona kwamba hakuna chochote kisicho cha kawaida kilichomtokea, wakabadili mawazo yao na kuanza kusema kwamba yeye ni mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wao wakadhani ya kuwa atavimba au kuanguka chini kwa kufa ghafula; na wakiisha kumwangalia sana, na kuona kwamba halimpati dhara lo lote, wakageuka, wakasema kwamba yeye ni mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wakadhani atavimba au ataanguka na kufa. Walisubiri na kumwangalia kwa muda mrefu, lakini hakuna kibaya kilichomtokea. Hivyo wakabadili mawazo yao. Wakasema, “Paulo ni mungu!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wale watu walikuwa wakitazamia kwamba angevimba au hapohapo angeanguka chini na kufa. Baada ya kungojea kwa muda mrefu bila kuona kwamba Paulo amepatwa na jambo lolote lisilo la kawaida, walibadilisha fikira zao juu yake, wakasema kuwa ni mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale watu walikuwa wakitazamia kwamba angevimba au angeanguka chini na kufa ghafla. Baada ya kungojea kwa muda mrefu bila kuona kwamba Paulo amepatwa na jambo lolote lisilo la kawaida, walibadilisha fikira zao juu yake, wakasema kuwa yeye ni mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu walikuwa wanangoja avimbe au aanguke ghafula na kufa. Lakini baada ya kungoja kwa muda mrefu na kuona hakuna cho chote kisicho cha kawaida kilichomtokea, wakabadili mawazo yao na kuanza kusema kwamba yeye ni mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu walikuwa wanangoja avimbe au aanguke ghafula na kufa. Lakini baada ya kungoja kwa muda mrefu na kuona kwamba hakuna chochote kisicho cha kawaida kilichomtokea, wakabadili mawazo yao na kuanza kusema kwamba yeye ni mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wao wakadhani ya kuwa atavimba au kuanguka chini kwa kufa ghafla; na wakiisha kumwangalia sana, na kuona kwamba halimpati dhara lolote, wakageuka, wakasema kwamba yeye ni mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale watu walikuwa wakitazamia kwamba angevimba au angeanguka chini na kufa ghafla. Baada ya kungojea kwa muda mrefu bila kuona kwamba Paulo amepatwa na jambo lolote lisilo la kawaida, walibadilisha fikira zao juu yake, wakasema kuwa yeye ni mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wale walimtunduia na kungoja, avimbe au aanguke chini akifa papo hapo. Lakini walipongoja sana na kuona, ya kuwa hapati kibaya cho chote, wakageuka na kusema: Yeye ni mungu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wao wakadhani ya kuwa atavimba au kuanguka chini kwa kufa ghafula; na wakiisha kumwangalia sana, na kuona kwamba halimpati dhara lo lote, wakageuka, wakasema kwamba yeye ni mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao watu wale walingojea kuona ikiwa atavimba mukono au ataanguka mara moja na kufa. Lakini kisha kungoja muda murefu na kuona kwamba hakupata hasara yoyote, wakabadilisha mawazo yao hata wakasema kwamba yeye ni mumoja wa miungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakamwangalia sana wakidhani ya kuwa atavimba au kuanguka chini, amekwisha kufa kwa ghafula; na wakiisha kumwangalia sana, na kuona kwamba halimpati dhara lo lote, wakabadili fikara zao, wakasema kwamba yeye ni Mungu.