Acts 3:10 — Compare Translations
13 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipomtambua kuwa ndiye yule aliyekuwa anaombaomba karibu na ule “Mlango Mzuri” wa hekalu, wakashangaa mno hata wasiweze kuelewa yaliyompata.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wakamtambua kuwa ni yule mtu aliyekuwa akiketi nje ya Hekalu penye lango liitwalo Zuri akiomba msaada, nao wakajawa na mshangao, wakastaajabu kwa yale yaliyomtukia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiketi na kuomba sadaka penye mlango Mzuri wa hekalu; wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walipomtambua kuwa ndiye yule aliyekuwa anaombaomba karibu na ule “Mlango Mzuri” wa Hekalu, wakashangaa mno hata wasiweze kuelewa yaliyompata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipomtambua kuwa ndiye yule aliyekuwa anaombaomba karibu na ule “Mlango Mzuri” wa hekalu, wakashangaa mno hata wasiweze kuelewa yaliyompata.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wakamtambua kuwa ni yule mtu aliyekuwa akiketi nje ya Hekalu penye lango liitwalo Zuri akiomba msaada, nao wakajawa na mshangao, wakastaajabu juu ya yale yaliyomtukia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wakamtambua kuwa ni yule mtu aliyekuwa akiketi nje ya Hekalu penye lango liitwalo Zuri akiomba msaada, nao wakajawa na mshangao, wakastaajabu juu ya yale yaliyomtukia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiketi na kuomba sadaka penye mlango wa hekalu uitwao Mzuri; wakawa na mshangao na kustaajabia mambo yale yaliyompata.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipomtambua kuwa ndiye yule aliyekuwa anaombaomba karibu na ule “Mlango Mzuri” wa hekalu, wakashangaa mno hata wasiweze kuelewa yaliyompata.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakamtambua, ya kuwa huyu ndiye aliyekaa na kuomba sadaka karibu ya Mlango Mzuri wa Patakatifu. Wote wakashangaa mno na kuyastukia yale yaliyompata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiketi na kuomba sadaka penye mlango Mzuri wa hekalu; wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipotambua kwamba yeye ndiye yule kiwete aliyekuwa akiikaa na kuombaomba musaada kwenye mulango wa hekalu unaoitwa “Muzuri,” wakashikwa na hofu na kushangaa sana na mambo yale yaliyomutokea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa ameketi na kuomba sadaka penye mlango mzuri wa hekalu: wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata.