Acts 3:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wote, wakiwa na mshangao mkubwa, wakaanza kukimbilia mahali palipoitwa “Ukumbi wa Solomoni,” ambapo yule mtu alikuwa bado anaandamana na Petro na Yohane.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Aliyeponywa alipokuwa akiambatana na Petro na Yohana, watu wote walishangaa mno, wakaja wakiwakimbilia pale Ukumbi wa Sulemani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi alipokuwa akiwashika Petro na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika tao lile lililoitwa tao la Sulemani, wakishangaa sana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Huku wakishangaa, watu wale waliwakimbilia Petro na Yohana pale walikokuwa katika Ukumbi wa Sulemani. Mtu yule aliyeponywa alikuwa akingali amewang'anga'nia Petro na Yohana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu wote, wakiwa na mshangao mkubwa wakaanza kukimbilia mahali palipoitwa “Ukumbi wa Solomoni,” ambapo yule mtu alikuwa bado anaandamana na Petro na Yohane.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wote, wakiwa na mshangao mkubwa, wakaanza kukimbilia mahali palipoitwa “Ukumbi wa Solomoni,” ambapo yule mtu alikuwa bado anaandamana na Petro na Yohane.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule mtu kiwete aliyeponywa alipokuwa akiambatana na Petro na Yohana, watu wote walishangaa mno, wakaja wanawakimbilia mpaka kwenye ukumbi wa Solomoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Aliyeponywa alipokuwa akiambatana na Petro na Yohana, watu wote walishangaa mno, wakaja wakiwakimbilia pale ukumbi wa Sulemani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi alipokuwa akiwashika Petro na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika tao lile lililoitwa tao la Sulemani, wakishangaa sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wote, wakiwa na mshangao mkubwa, wakaanza kukimbilia mahali palipoitwa “Ukumbi wa Solomoni,” ambapo yule mtu alikuwa bado anaandamana na Petro na Yohane.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Aliposhikamana na Petero na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika ukumbi unaoitwa wa Salomo kwa kushangaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi alipokuwa akiwashika Petro na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika tao lile lililoitwa tao la Sulemani, wakishangaa sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu huyo hakutaka kuachana na Petro na Yoane. Kwa hiyo watu wote wakashangaa sana na kukimbilia kwenye baraza la hekalu wanaloita La Solomono.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi yule kiwete aliyeponywa alipokuwa akiwashika Petro na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika tao lile lililokwitwa tao la Sulemani; wakishangaa sana.