Acts 3:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jina la Yesu na imani katika jina hilo ndivyo vilivyompa nguvu mtu huyu mnayemwona na kumfahamu. Imani kwa Yesu ndiyo iliyomponya kabisa mtu huyu kama mnavyoona nyote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa imani katika jina la Isa, huyu mtu mnayemwona na kumfahamu ametiwa nguvu. Ni jina la Isa na imani kutoka kwake ambayo imemponya kabisa huyu mtu, kama nyote mnavyoona.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Huyu mlemavu wa miguu ameponywa kwa sababu tunalo tumaini katika Yesu. Nguvu ya Yesu ndiyo iliyomponya. Mnamwona na mnamfahamu mtu huyu. Ameponywa kabisa kwa sababu ya imani inayotokana na Yesu. Ninyi nyote mmeona hili likitokea!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Jina la Yesu na imani katika jina hilo ndivyo vilivyompa nguvu mtu huyu mnayemwona na kumfahamu. Imani kwa Yesu ndiyo iliyomponya kabisa mtu huyu kama mnavyoona nyote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jina la Yesu na imani katika jina hilo ndivyo vilivyompa nguvu mtu huyu mnayemwona na kumfahamu. Imani kwa Yesu ndiyo iliyomponya kabisa mtu huyu kama mnavyoona nyote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa imani katika jina la Yesu, huyu mtu mnayemwona na kumfahamu ametiwa nguvu. Ni kwa jina la Yesu na imani ile itokayo kwake ambayo imemponya kabisa huyu mtu, kama ninyi wote mnavyoona.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa imani katika jina la Isa, huyu mtu mnayemwona na kumfahamu ametiwa nguvu. Ni kwa jina la Isa na imani itokayo kwake ambayo imemponya kabisa huyu mtu, kama ninyi wote mnavyoona.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jina la Yesu na imani katika jina hilo ndivyo vilivyompa nguvu mtu huyu mnayemwona na kumfahamu. Imani kwa Yesu ndiyo iliyomponya kabisa mtu huyu kama mnavyoona nyote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena kwa hivyo, huyu alivyolitegemea Jina lake, hilo Jina lake limemtia nguvu huyu, mnayemwona na kumjua. Kweli hivyo, alivyolitegemea kwa kutiwa nguvu nalo, ndivyo vilivyompa huu uzima wote, mnaouona ninyi nyote.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu huyu munayemujua na kumwona amepata tena nguvu kwa uwezo wa jina la Yesu, kwa njia ya kuaminia jina hili. Yeye amepona kabisa sawa vile ninyi wote munavyojionea, kwa njia ya kumwaminia Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kwa imani ya jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnaemwona na kumjua: na imani ile iliyo kwa njia yake yeye imempatia huyu mbele yemi ninyi nyote uzima huu mkamilifu.