Acts 3:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa maana Mose alisema, ‘Bwana Mungu wenu atawapelekeeni nabii kama mimi kutoka kati yenu nyinyi wenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana Musa alisema, ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Itawapasa kumtii huyo kwa kila jambo atakalowaambia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana Musa kweli alisema ya kwamba, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye katika mambo yote atakayonena nanyi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Musa alisema, ‘Bwana Mungu wako atakupa nabii. Nabii huyo atatoka miongoni mwa watu wako. Atakuwa kama mimi. Ni lazima mtii kila kitu atakachowaambia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa maana Mose alisema, Bwana Mungu wenu atawapelekeeni nabii kama mimi kutoka kati yenu ninyi wenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa maana Mose alisema, ‘Bwana Mungu wenu atawapelekeeni nabii kama mimi kutoka kati yenu nyinyi wenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana Mose alisema, ‘Bwana Mungu wenu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu, itawapasa kumtii huyo kwa kila jambo atakalowaambia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana Musa alisema, ‘Bwana Mwenyezi Mungu wenu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Itawapasa kumtii huyo kwa kila jambo atakalowaambia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana Musa kweli alisema ya kwamba, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye katika mambo yote atakayonena nanyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa maana Mose alisema, ‘Bwana Mungu wenu atawapelekeeni nabii kama mimi kutoka kati yenu nyinyi wenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose alisema: Miongoni mwa ndugu zenu Bwana Mungu atawainulia mfumbuaji atakayelingana na mimi, nanyi sharti mmsikie yote, atakayowaambia!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana Musa kweli alisema ya kwamba, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye katika mambo yote atakayonena nanyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana Musa alisema: ‘Bwana Mungu wenu atawatumia ninyi nabii anayekuwa sawa mimi, toka katika taifa lenu. Nanyi mutasikiliza mambo yote nabii yule atakayowaambia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana Musa aliwaambia baba zetu ya kama, Bwana Mungu atawainulieni nabii, atakaetoka katika ndugu zenu, kama mimi, msikieni yeye katika mambo yote atakayonena.