Acts 3:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mungu alimfufua mtumishi wake kwa faida yenu kwanza, akamtuma awaleteeni baraka kwa kumfanya kila mmoja wenu aachane kabisa na maovu yake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu alipomfufua Isa Mwanawe, alimtuma kwenu kwanza, ili awabariki kwa kumgeuza kila mmoja wenu kutoka njia yake mbaya.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu amemtuma Yesu, mtumishi wake maalumu. Alimtuma kwenu kwanza, ili awabariki kwa kuwageuza kila mmoja wenu aache njia zake za uovu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, ilikuwa kwa ajili yenu kwanza kwamba Mungu alimfufua mtumishi wake, alimtuma awabariki kwa kumfanya kila mmoja wenu aachane kabisa na maovu yake.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mungu alimfufua mtumishi wake kwa faida yenu kwanza, akamtuma awaleteeni baraka kwa kumfanya kila mmoja wenu aachane kabisa na maovu yake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu alipomfufua Yesu Mwanawe, alimtuma kwenu kwanza, ili awabariki kwa kumgeuza kila mmoja wenu kutoka katika njia yake mbaya.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu alipomfufua Isa Mwanawe, alimtuma kwenu kwanza, ili awabariki kwa kumgeuza kila mmoja wenu kutoka njia yake mbaya.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabariki kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mungu alimfufua mtumishi wake kwa faida yenu kwanza, akamtuma awaleteeni baraka kwa kumfanya kila mmoja wenu aachane kabisa na maovu yake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninyi m wa kwanza, Mungu aliowafufulia mtoto wake na kumtuma, awabariki, mgeuke kila mmoja mkiyaepuka mabaya yenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivi Mungu alimutuma mutumishi wake kwa ajili yenu kwanza, kusudi awabariki ninyi, akimugeuza kila mumoja wenu toka katika njia zake mbaya.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, illi kuwabarikini kwa kumwepusha killa mmoja wenu na maovu wake.