Acts 4:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wokovu haupatikani kwa mtu mwingine yeyote, kwa maana duniani pote, binadamu hawakupewa jina la mtu mwingine ambaye sisi tunaweza kuokolewa naye.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wala hakuna wokovu katika mwingine yeyote, kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu linalopasa kutuokoa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu peke yake ndiye anayeweza kuokoa watu. Jina lake ndiyo nguvu pekee iliyotolewa kumwokoa mtu yeyote ulimwenguni. Ni lazima tuokoke kupitia yeye!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wokovu haupatikani kwa mtu mwingine yeyote, kwa maana duniani pote, binadamu hawakupewa jina la mtu mwingine ambaye sisi tunaweza kuokolewa naye.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wokovu haupatikani kwa mtu mwingine yeyote, kwa maana duniani pote, binadamu hawakupewa jina la mtu mwingine ambaye sisi tunaweza kuokolewa naye.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hakuna Jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wokovu haupatikani kwa mtu mwingine yeyote, kwa maana duniani pote, binadamu hawakupewa jina la mtu mwingine ambaye sisi tunaweza kuokolewa naye.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena hapana pengine panapopatikana wokovu, wala hapana Jina jingine chini ya mbingu, sisi watu tulilopewa, tuokoke nalo.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Hivi hakuna anayeweza kuokolewa kwa njia ya mutu mwingine yeyote, kwa maana katika dunia nzima hakuna jina lingine lolote watu walilopewa lenye uwezo wa kuwaokoa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wala hakuna wokofu katika mwingine aliye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wana Adamu litupasalo kuokolewa nalo.