Acts 4:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini ili tupate kuzuia jambo hili lisienee zaidi kati ya watu, tuwaonye wasiongee na mtu yeyote kwa jina la Yesu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ili kuzuia jambo hili lisiendelee kuenea zaidi kwa watu, ni lazima tuwaonye watu hawa ili wasiseme tena na mtu yeyote kwa jina la Isa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini neno hili lisije likaenea katika watu, na tuwatishe wasiseme tena na mtu awaye yote kwa jina hili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini ni lazima tuwatishe ili wasiendelee kuwaambia watu kutumia jina lile. Ili tatizo hili lisisambae miongoni mwa watu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini ili tupate kuzuia jambo hili lisienee zaidi kati ya watu, tuwaonye wasiongee na mtu yeyote kwa jina la Yesu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini ili tupate kuzuia jambo hili lisienee zaidi kati ya watu, tuwaonye wasiongee na mtu yeyote kwa jina la Yesu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ili kuzuia jambo hili lisiendelee kuenea zaidi miongoni mwa watu, ni lazima tuwaonye watu hawa ili wasiseme tena na mtu ye yote kwa jina la Yesu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ili kuzuia jambo hili lisiendelee kuenea zaidi kwa watu, ni lazima tuwaonye watu hawa ili wasiseme tena na mtu yeyote kwa jina la Isa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini ili neno hili lisije likaenea katika watu, na tuwatishe wasiseme tena na mtu yeyote kwa jina hili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini ili tupate kuzuia jambo hili lisienee zaidi kati ya watu, tuwaonye wasiongee na mtu yeyote kwa jina la Yesu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kusudi isipate kuenea po pote kwa watu, tuwatishe, wasimwambie tena mtu ye yote jambo lo lote la Jina hilo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini neno hili lisije likaenea katika watu, na tuwatishe wasiseme tena na mtu awaye yote kwa jina hili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kwa kuzuiza habari za jambo lililotokea zisisambae zaidi kati ya watu, tuwakataze kwa ukali wasiendelee tena kusema na mutu yeyote wakitaja jina la Yesu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini neno hili lisije likaenea katika watu, tuwaogofishe wasiseme tena na mtu aliye yote kwa jina hili.